Mama eti na sisi Baba yetu anakufa lini?

Takari ya Leo

MAMA BABA YETU NAYE ATAKUFA LINI

Hakuna siku niliyojisikia vibaya kama siku moja nipo nyumbani, kama kawaida yangu nilikua nimelewa chakari, nimejilaza kwenye kochi. Hapo ni baada ya kumtukana mke wangu na kuwaambia wote waende jikoni.

Ilikua ni usiku, lakini baada ya muda njaa ilinibana, nilinyanyuka kwa kuyumbayumba kwenda jikoni ili kudai chakula ambacho mke wangu amepika nikiwa hata sijui pesa katolea wapi kwani asubuhi sikuacha chochote.

Baada ya kufika mlangoni nikiwa kabla sijaupiga teke kama kawaida yangu nilisikia sauti ya mtoto wangu wa miaka minne akimuuliza Mama yake. “Mama eti na sisi Baba yetu anakufa lini?”

Nilistuka, nikasimama na kuanza kusikilzia walikua wanazungumza nini. “Wewe mtoto nyamaza usiseme hivyo ni vibaya, tema mate chini!” Mke wangu alimkemea lakini mtoto hakujali.

“Sasa Mama mbona Dadada amesema Baba yake Juma amekufa, ameenda kwa Mungu na hatarudi tena, kwanini na sisi Baba yetu asiende ili tubaki wenyewe…”

Mtoto aliendelea kuongea, mke wangu alijaribu kumkanya lakini hakusikia aliendelea. Mtoto mwingine mkubwa binti yangu wa miaka kumi yeye alimkatisha kumuelewesha.

“Baba Juma anaenda kwa Mungu kwasababu ni mtu mzuri, Baba yeye hataenda kwa Mungu anaenda kwa shetani, haendi mbinguni….” Alimaliza kumuelewesha mdogo wake, mke wangu alichanganyikiwa zaidi, alijaribu kuwakanya lakini yule mdogo aliendelea…

“Heri Baba hata afe, maana anakupiga wewe kila siku ana sisi kutupiga. Mimi ningekua Rambo ningemuua paaap! Paaa! Pigo moja tu anakufa! Nikiwa mkubwa namuulia mbali” Alionge akwa kujigamba.

Mtoto aliendelea kuongea sasa kwa msisimko. Nilijikuta nasimama wima, pombe zote ziliniishia njaa ilikoma, nilianza kutembea kurudi sebuleni, nilishindwa hata kukaa. Niliingia chumbani na kuanza kujiangalia kwenye kioo.

Nimeyafanya nini maisha yangu. niliwaza nikikumbuka zamani nilivyokua nikitamani kuwa na familia nzuri, kua na mke mzuri na watoto ambao wananipenda.

Lakini sasa mtoto wangu mwenywe, mtoto wa miaka minne alikua anatamani mimi Baba yake kufa! Nilitamani kulia lakini nilijua haitasiadia, niliingia bafuni na kuanza kujitapisha, nilitapika pombe yote, nikaingia kwenye friji nikachukua bia zote na wine.

Nikaenda kuzimwaga kisha nikarudi jikoni, nikafungua mlango kistaarabu nikaumbaia mke wangu sasa nimecha pombe, naomba mnisamehe lakini sasa nimemaua kubadiliaka.

Tangu siku hiyo sijawahi kunywa pombe, kumpiga wala kumtukana mke wangu, nina amani na furaha kuliko kipindi chote. Kumbe manaynyaso niliyokua nikimpa mke wangu yalikua yakiniumiza mimi zaidi kuliko mke wangu.

***MWISHO

Kamwe hakuna furaha ya peke yako, huwezi kufurahi ukiwa mwenyewe, starehe ya peke yako ni starehe ya upweke. Mwanaume unahitaji familia ili uweze kusema unafuraha.

Kama familia yako inalia, mkeo analia basi jua huna furaha. Pia haikufanyi mwanaume kamili, haikufanyi mwanaume zaidi kuwatesa wanao au mke wako, inakufanya mwanaume mpumbavu tu!

Kama wewe ni baba jiulize je kwa unayotenda ipo siku mwanao atayasema haya?

He he he Kwenye kioo ulikuwa unajiangalia jinsi ulivokuwa kolo?
 
KWA MAANA HII WATU WANAOKUNYWA POMBE NA KUJIDAI HAWAWEZI KUACHA HUWA WANAJIENDEKEZA? HAWAJAPA SABABU TU YA KUACHA, MAANA MIMI HATA SIJUI POMBE INA LADHA GANI TOKA NIZALIWE, ILA NAWAONE HURUMA SANA WANYWAJI WASIOJIWEZA
 
Hadithi nzuri,Ila umenikera kumwaga bia na wine[emoji15]
 
Kama ndo mm ningekamata hako katoto kanakotaka nife ningekavuta mashavu hdi yachomoke" hukua umelewa wewe vijimaneno vya mtt Wa miaka minne vimekulegeza ,umetuaibisha walevi wenzio sio vbaya ukitutaka radhi
 
Huyo baba, alikuwa na tabia za kupiga tu mkewe. Hivyo akiutwika, alikuwa anaongeza sumu ya ugomvi. Nina fahamu wanywaji wengi tu, ambao wakubwa vileo, na wanarudi nyumbani salama, hawafanyi fujo, wanawasikiliza wenzi wao na watoto bila ugomvi. Kunywa kileo kwa kiasi kwa manufaa ya jamii nzima.
 
kweli mpo tofauti, sie baba yetu akinywa ndiyo muda mzuri wa kupiga nae story, akiwa mzima ataishia tu kusema aiseee. kamaliza haongeagi kabisa.
 
Wanaume wengi ni selfish;atataka akitoka kazini aende sehemu nzuri kabisa na marafiki zake;aburudike kwa vinywaji na nyama choma na muziki laini.
Akija nyumbani usiku atakuwa mkali kama pilipili;hataki kelele;hana story.Atakula kwa kuzuga vijiko viwili vitatu vya wali maharage na kwenda kulala.
Pombe sio mbaya;mbaya mwanadamu siku zote.
Kama pombe inaibua demons wako wabaya achana nayo!
Nakemea ulevi!
 
Back
Top Bottom