Duuuu we kaka, yani nafasi ya mke kwako ni ipi?
Umemuoa kwa sababu ya mama yako, au kwa sababu yako na yeye muendeshe maisha. Kwanza nakuhakikishia maisha unayoishi na mkeo sio ya furaha kabisa, haiwezekani mama wa watoto wako hajui kipato chako, hajui unachopata na unachopoteza. Nasikia hsira gafla.
Kaka naomba nikuulize swali hivi ukipanda hiyo ndege halafu kwa bahati mbaya usifike huko unakokwenda, mama yako ndo atasimamia miradi yako na kukulelea watoto wako? Unamweka huyo mkeo ktk mazingira gani, si ndio atafukuzwa na watoto wake kama mbwa??
Biblia inasema hivi, mtu ataachana na mama yake na baba yake, nao watakuwa mwili mmoja, alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe. Asomaye na afahamu. Naishia hapa nitarudi tena.
Hehehe thanx lizzy naona umekuja juu.
Wife bado anapiga kitabu na anaakili sana. Hatakua anaenda kuomba hela coz nimeset kiwango flani kiwe debited kwangu nakuwa credited kwake.
Lakini unajua nyie mabinti mnadharau na kudanganyika kirahisi sana. Kutokana na hivyo unaweza kuta akadanganyika na kushawishika maana anajua kwa uhakika limit ya mumewe no matter how big or small.
kwa kweli hata mimi nimeshangaa, na hii inadhihirisha ni jinsi gani wanawake bado tunanyanyasika kwenye ndoa. hii ni sawasawa na kuhalalisha kama ukifa leo mkeo anyang'anywe kila kitu na mama yako au ndugu zako. imeniumiza sana hii aisee
Habari wakuu. Naomba tubadilishane mawazo kwa hili.
Naenda kusoma nje. Mshahara wangu utaendelea kuingia kwenye akaunt yangu ambayo nayo ndio naitumia kwa biashara zangu. Sasa navyoondoka sijui kadi nimpatie mama au mke kwa ajili ya kuendelea ku run shughuli na matumizi mengine. Wife hajui kipato changu taslimu na ni vizuri,ila kwenda kuomba kwa mama inaweza ikawa kero.
Mwalioneje hili?
Yani mpendwa, najaribu kupiga picha huyo mke anajisikia je tu. Manake sio kwamba hakimuumi, na huyo jamaa hana hata marafiki wa kiume wakamshauri!!! Au rafiki ake mkubwa ni mama yake. Daaa wanawake tufanye kazi hii habari ya kuolewa na mtu anakunyanyasa kisa huna kitu haikubaliki!!!!
Babu wakati natuma post hii sikujua kuwa naweza badilishwa mawazo ndani ya JF haraka hivyo. Pamoja na kua lizzy,LD etc wamejibu kwa hasira sana ila nimewaelewa na hasira zao zimesaidia uelewa huo.Kumuachia Bank card yako mama yako si sawa hata kidogo na ni kumdhalilisha mkeo na inaweza kusababisha ndoa yako kuingia matatani(nategemea huyu ni mke wa ndoa). Sijakupata hapo uliposema mkeo hajui kipato chako na ni vizuri. Je, kuna sababu yoyote iliyokufanya kutoona umuhimu wa mkeo kujua kipato chako?
Ok,ok punguzeni jazba wapendwa najua ni topic inagusa. Please twendeni pole pole.
Nampenda sana mke wangu mpaka watu wapumbavu wanasema nimelogwa. Hii ya wife ku run shughuli naona itampa wakati mgumu kwa kasociety kangu kakijinga kanakozua hayo mambo ya kulogwa. Halafu hatuishi kwenye kisiwa hii society ikimkataa wakati sipo ataishije?
VoA asante I am thinking or at least i'm thinking that i'm thinking. Get it? Lol.

Babu wakati natuma post hii sikujua kuwa naweza badilishwa mawazo ndani ya JF haraka hivyo. Pamoja na kua lizzy,LD etc wamejibu kwa hasira sana ila nimewaelewa na hasira zao zimesaidia uelewa huo.
Ndoa yetu ni changa 1 year and a few months. Kuna haja gani ya yeye kujua mshahara kama kila atakacho apata na nikishindwa humueleza?

Ni Bubu siyo Babu hahahahahah. Ndani ya ndoa hakutakiwi kuwe na siri ya aina yoyote ile ikiwemo kipato cha wahusika. Mara tu ndani ya ndoa yeyote ile mmoja wa wahusika akianza kutaka kufichaficha mambo yake basi hapo ndipo matatizo huanzia na hata kuzua balaa ndani ya ndoa.