msalala kwetu
Member
- Jan 29, 2016
- 71
- 72
Wakuu habari zenu,
Mwaka 2012 nilienda kozi nje ya nchi kwa miezi 3 hapa hapa Africa, nyuma niliacha mke na watoto wawili walio primary school,
nikiwa kozi rafiki yangu akawa anakwenda kulala kwangu mara kwa mara especially weekends, akawa analala chumbani kwangu, haijajulikana hadi leo walianza lini uhusiano huo, alikua akienda kwangu kwa gia ya kuwaona wanaendeleaje.
Niliporudi, nikakuta wife kamtimua kazi house girl wetu bila maelezo ya kueleweka, nikapuuzia, baadae rafiki kipenzi wa wife wa tangu shule na ambae wanasali jumuia moja maana amepanga mitaa yetu, akaniambia kwa urefu uhusiano wa wife na mshikaji wangu, ila kwa sharti la kutomtaja whatsoever the case.
Baadae nikaona niende kumtafuta yule housegurl aliefukuzwa kazi na wife nikampata, aka confirm habari zile na kunieleza kwa kirefu na ndio kisa cha yy kufukuzwa kazi pale kwangu baada ya kumuhoji kuwa " kwanini unamfanyia shemeji matendo haya.
Baada ya kujiridhisha nikamuita wife mbele ya wazazi wake na kueleza kila kitu akabaki kimya akilia, nikamkabidhisha kwa wazee wake hapo hapo, akiwa kwao aliendelea kunibembeleza na kuniomba msamaha kwa kutuma watu mbali mbali wenye heshima, sikurudi nyuma, akasafiri kijijini kwetu kuwaona wazazi wangu na kuwaangukia, alikaa huko mwezi mzima.
Baadae wakaja wote na wazazi wangu hadi kwangu, wakasema pamoja na yote yaliyotokea niishi nae hivyo ametubu, sio ombi ni amri ndio maana wamemleta wao, moyoni nikasema najua cha kufanya, nilishindwa kuwaelewa, wanamtetea mtu ambae ameniumiza despite kuwa nilimuachia kadi ya benki awe anachukua mshahara wangu kuendesha familia, mimi kule kozi nikawa naishi kwa chakula cha kulipiwa na posho kidogo tu.
Wazazi walipoondoka tu, nikaanza kumfanyia visa na matendo mabaya ili aondoke, nikatafuta msichana wangu nikawa najiachia nae pale mtaani bila woga, nakunywa nae bar za mtaani, nikaanza kuja nae home nalala nae chumba kingine, akawa anatufanyia fujo lakini namdhibiti kiume hadi tunajifungia chumbani, nilikua nafanya haya yote ili wife aondoke lakini wapi, yupo tu, anawapigia simu wazazi kushitaki wakinipigia nawaambia huyu ni mke wenu mimi nilimtimua nyinyi mkamleta tena, ni mke wenu.
Tumeishi kwa hali hii tangu 2012 hadi sasa, yule msichana wangu akachoka hizi vurugu akaamua kuniacha, sasa nina mwingine, sina uhakika kama yupo mwanamke huko nje angeweza kuvumilia matendo niliyomtendea huyu wife, lengo ni aondoke lakini hataki kuondoka hata baada ya kumu offer kugawana mali, watoto wameathirika sana na hizi vurugu huwa nikiwapeleka kwa dada yangu wanakataa kurudi
Lakini yote haya aliyasababisha yeye kwa tamaa, nilishamueleza tangu siku ya ndoa kanisani kuwa nitakusamehe yote lakini uzinzi huwa sisamehi, sijamgusa tangu 2012.
Wadau naombeni ushauri nimtoe vipi huyu mwanamke?
Au mnadhani ipo siku naweza kusahau usaliti wake na kumpenda?
Na kama ni kumuacha ndani tutaishi hivi hadi lini?
Kuhusu watoto mnaonaje niwaache uko uko kwa dada yangu walelewe huko wasomee huko huko? Maana tangu likizo ya December wamekatalia huko hivyo school bus huwa linawafuata huko badala ya kwangu.
Nitaheshimu mawazo yenu as my last resort.