Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,471
- 23,744
" Mimi ni kijana wa miaka 32 nimeajiriwa namshukuru Mungu kipato changu kipo vizuri sina matatizo toka miaka miwili iliyopita nilimpata dada mmoja ambaye niliridhia awe mke wangu mtarajiwa.alikuwa akisoma nikampa muda amalize chuo ili baada ya hapo tuanze michakato ya ndoa.
Nlimpeleka kwa wazazi wangu baba alikuwa nje ya nchi kwa muda mrefu hivyo mama ndiye aliyefanikiwa kupata muda wa kumwona na kuongea naye baadaye alipomaliza chuo nilienda kwa mama kumwambia sasa ni wakati muafaka nataka kujitambulisha kwao huyo msichana cha kustaajabisha mama alibadilika sana na kusema huyo msichana yeye hajampenda.
Tulikuwa na maongezi marefu sana nikitaka kujua kwa nini hajampenda hakuweza toa sababu yoyote ile zaidi ya kusema hajamwingia moyonibsuala hili nilikuja kumshirikisha baba alipotoka safari alionekana kulikubali lakini alipoenda kuongea na mama alirudi amebadilika naye anaunga mkono anachosema mama ingawa hajawai mwona huyo msichana hata siku moja.
Siku zikaenda mgogoro ukiwa mkubwa mpaka siku moja ya kikao mama akaja kunambia yeye kuna binti ambaye ndo anapendekeza nimwoe akanitajia huyo binti ambaye ni mtoto wa rafiki yake kiukweli namfahamu huyo binti na toka nimemwona sikuwahi kujenga naye hisia hata siku moja sikuwahi mfikiria kuwa hata mpenzi au kusema kuwa kuna siku nitakuwa na hamu ya kusex naye nilimwambia mama kuwa huyo binti mimi sijamuafiki.
Mama aliendelea kusisitiza kuwa huyo ndiye chagua sahihi lakini nachowaza kuwa ni chaguo sahihi kwake si kwangu nami nahitaji mtu ambaye awe sahihi kwangu kama mapungufu basi yasemwe yaliyopo ya huyu wasiyemtaka lakini pia hata mimi nina mapungufu yangu kwanini wasinambie kwanza ya huyo msichana ili nipime halafu niamue mwenyewe?
Zaidi ya mwaka sasa tumekuwa na ukinzani huo bahati mbaya sana baba ni msomi na mama ni msomi pia maisha yao yoote wanaishi mjini na wamefanikiwa kutembea hata nchi za nje kwanini waje na mawazo haya ya kizamani?binafsi nimefikia hatua nasema pengine nisije kuoa kabisa au niondoke nikaanze maisha yangu peke yangu na huyo dada nikikata mawasiliano nao kabisa.
Maana mama anasisitiza kuwa nikimwona huyu yeye hatofika hata nyumbani kwangu ni kama ametengeneza chuki naye ambayo siielewi inatoka wapi kaamua kumchukia kabisa na kusingizia mengi kuwa huyo binti familia yake ni wachawi wakati huyo dada familia yake ipo mbali na jiji la dar unapita mikoa mingine kadhaa kufika huo uchawi ni upi?
Ok kama anasema kuwa binti huyu ana madhaifu mbona nikimwambia yeye au baba wanitajie hawataji lolote zaidi ya kusema tu hawamtaki? ni jambo ambalo limenitesa nimefikia hatua mbayo sielewi mwisho wake ni nini maana ni mgogoro wa kifamilia ambao unanifanya nianze hata kuwachukia wazazi wangu maana ni kama wamedhamiria kunitesa,kuniumiza pasipo sababu.
Nipo njia panda nawaza niondoke nyumbani nikaanze maisha sehemu isiyojulikana kwao?nikate mawasiliano nao kabisa?mimi binafsi niende huko kwa wazazi wa huyu binti nikajitambulishe na kuanza akufuata process nyingine zote pasipo wazazi wangu?au ndo niamue kabisa kuachana na habari za kuoa niishi tu bila mke? maana huyu dada katika uhusiano wetu wa zaidi ya miaka miwili tumefanya mengi sana tumesaidiana mengi kiasi kwamba ni ngumu leo hii kumwacha nianze maisha mapya na mwanamke mwingine.
Na yeye ameshakataa kwao wachumba zaidi ya watano akiamini mimi naye tutaoana nifanye nini katika jambo hili ndugu zanguni nimekata tamaa sana na sitamani kuendelea kuteseka katika jambo hili."
msaada wa maoni na ushauri kwa kijana mwenzenu.