Mama mmoja ajulikanae kwa jina la Asma akitoa maelezo Leo(20/4/2017) katika kipindi cha power breakfast cha clouds FM,amelalamika kuibiwa mtoto wake mmoja baada ya kujifungua kwa operation katika hospitali ya wilaya Temeke. Amesema vipimo vyote vya ultrasound alivopima sehemu mbili tofauti ikiwepo Temeke hospitali vilionyesha kuwa ana watoto mapacha, na alivoenda Temeke docta mmoja aliyemtaja kwa jina la Dr. Elisha alimpima ultrasound akagundua kuwa mtoto mmoja ameziba njia na mwingine amekaa vizuri hivyo akaamuru afanyiwe operation. Wakati yuko theatre doctor MWANAMKE aliyehusika katika operation kabla ya kufanya operation akamwambia Asma kuwa ana mtoto mmoja tu akidai kuwa ultrasound imedanganya.
Nimeandika kwa kifupi lakini kiujumla kitengo cha uzalishaji cha hospitali hii ni jipu. Nakumbuka Dada yangu pia alijifungulia hapo hospitali na aliombwa rushwa ndipo akapewa huduma.
Hii hospitali iangaliwe kwani ni shida, kwa wale ambao washawai kukutana na haya matatizo atakubaliana na Mimi.