Asalaam aleykum kwa ndugu zangu waislam.......bwana yesu asifiwe kwa ndugu zangu wakristo wale wengine kwemaaaaa ? bila shaka itifaki imezingatiwa . ndugu zangu napenda kuwambia tukio lililotokea Mbezi beach Siku ya Jana mama mmoja asiye na haibu hata chembe akitekeleza ile kauli ya hapa kazi tu kwa kuvamia Nyumba ya jirani yake huyu mama ni straiker WA hatari akaingia kwenye hiyo yumba akakuta Gari aina ya RAUM NEW MODEL MPYA na kuanza kuvunja vioo kisha kuanza kung'oa taa za gari, power window, na vifaa vingine kibao na kutokomea navyo kisha kwenda kuviweka nyumbani kwake akisubiraia kuvitafutia mteja ndipo wenyewe walivyo amka asubuhi na kukuta Gari likiwa jeupe limeibiwa vitu bila kumjua mchawi ni nani ndipo akatokea jirani mmoja na kuwatonya kua kuna MTU anamuhisi wahusika wakenda kutoa taarifa kituo cha police na kuja kufanya upekuzi na kumkuta akiwa na mzigo WA maana. Ina sikitisha sana kuona mama kama huyu anakuwa na mambo ya wizi kama haya sijui watoto wake wanajisikiaje dah inasikitisha sana mama yupo mbaloni analia tu. NATAMANI KU UPLOAD NA VIDEO YA GARI LILILOFANYIWA WIZI HUO LAKINI NASHINDWA
Mama kweli kafanya shoo ya kibabe, jeshi la mtu mmoja, kama naiona RAUM alivyoiacha uchi.
Kweli ni mwizi, tena jambazi na simtetei kabisa, ila apewe sifa yake kwa shoo aliofanya, kama amefanya peke yake basi ni noma. Anaweza akapindua hata serekali huyu mtu.
Mahakama itaamua.Inategemea vitu hivyo vimekutwa wapikwani inawezekana mtonyaji ndio kamchomekea kama aliona vikiibwa kwanini hakutoa taarifa wakati huo huo.Ndani ya jamii kuna chuki na visasi vya kutisha, ngoja wapelelezi wafanye kazi