Mama aeleza askari wa wanyamapori walivyombaka


Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Messages
13,488
Likes
27,322
Points
280
Age
48
Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2015
13,488 27,322 280
IMG_20171109_123957-620x308.jpg


MWANAMKE mmoja mkazi wa Kijiji cha Arash Tarafa ya Loliondo, wilayani Ngorongoro, Arusha, Nondomoli Saile, ambaye ameathirika na vitendo vya ubakaji wakati wa operesheni ondoa wafugaji wilayani humo amesema ipo haja ya waliohusika kukamatwa.

Nondomoli amesema haya ikiwa ni siku chache tangu Waziri wa Maliasili Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, kusitisha operesheni hiyo, baada ya kupokea taarifa za ukiukwaji wa sheria za vijiji na uwepo wa minong’ono kwamba operesheni hiyo iliendesha na watendaji wa mamlaka za hifadhi kwa kutekeleza matakwa ya muwekezaji.

Chanzo cha mgogoro huo kimetokana na Mamlaka za Hifadhi, kutaka kumega eneo la kilometa 1,500 la vijiji vilivyopo mpakani mwa hifadhi ya Serengeti ili kupafanya Pori Tengefu, jambo ambalo lilizua hali ya taharuki katika eneo hilo hadi pale Waziri Dk. Kigwangala alipoingilia kati kwa kusitisha operesheni hiyo Oktoba 27.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa wananchi wa vijiji vilivyoathirika na operesheni hiyo, mama huyo amesema wanawake wengi wanaishi na mawazo hadi leo baada ya kufanyiwa vitendo hivyo huku wengi wao wakishindwa kupata tiba kutokana na kuona aibu ya kueleza namna walivyofanyiwa ukatili huo kwa watu.

“Unajua kwa mila na desturi za kimasai ni aibu sana kwa mwanamke kueleza mtu namna ulivyobakwa na hivyo wengi nikiwemo mimi tumeamua kukaa kimya na wala hatujui hao waliotufanyia vitendo hivyo kama wana magonjwa au la na pia huenda hata wengine wamepata mimba.

“Tunachokiomba hapa ni serikali hasa kupitia huyu Waziri wa sasa wa Maliasili alioonesha nia njema ya kulitafutia suluhu mgogoro huu wa Loliondo kuwawajibisha na maaskari waliohusika kutufanyia vitendo hivyo wanawake na kuwafanya kuishi kwa mawazo hadi leo kwa kuwa ni mambo ambayo hayatoki akilini mapema,” ameshauri mama huyo.

Akielezea namna alivyofanyiwa vitendo hivyo vya ukatili, Nondomoli amesema anakumbuka ilikuwa Septemba 19 mwaka huu, asubuhi, askari wa hifadhi walipofika kwenye boma lao na kuwata watoke wote nje ili waweze kuliteketeza na moto.

Hata hivyo mwanamke huyu amesema wakati anajaribu kwenda kuokoa baadhi ya mali, ndipo mmoja wa askari alimkamata na kumbaka na kumsababishia maumivu kwenye maeneo ya mwili wake.
 
SK2016

SK2016

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2017
Messages
3,554
Likes
4,382
Points
280
SK2016

SK2016

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2017
3,554 4,382 280
Duh! Hatari sana.
Kipindi hiki cha awamu ya 5 mtu askari unabaka?
 

Forum statistics

Threads 1,235,534
Members 474,641
Posts 29,225,809