Malware and threat Browser Extensions

Malware and threat Browser Extensions

ymollel

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Posts
3,095
Reaction score
2,294
Je Computer yako imekuwa Slow ghafla?...
Kama wewe ni mtumiaji wa internet sana, haswa haswa kama unapenda kuDownload Pirated SOftware, (KeyGens,Activators,Loaders... etc). Software hizi nyingi zinaonekana kuwa Bure, lakini nyingi zinaunganishwa (Embedded) na Malware /Spyware/adware,worms au virus kwa ujumla. Kuna baadhi ya Malware/adware ambao kazi yao ni kukuletea Matangazo (Adds) kwenye Browser yako, kila unapoclick mahali inaleta POP-UP ya tangazo, wakati mwingine hata inaharibu Layout ya web-Page unayoitembelea kwani inachomeka matangazo ovyo ovyo bila mpangilio.

Hawa malware/adware wanachofanya ni kuInstall Extensions/Addons/Plugins kwenye Browser yako, na usipokuwa makini utajikuta wewe kazi yako ni kufunga POP-UPS na kuangalia matangazo.

Je Utafanyaje?
1. Ingia kwenye Control Panel-Add/Remove Programs, Angalia program yoyote ambayo huitambui, au hukuiweka wewe na uitoe. Na kama kuna program ambayo unawasiwasi nayo ila huielewi basi Google hilo jina kabla ya kuitoa.

2. Fungua kila Browser unayotumia , Nenda kwenye Settings->EXTENSIONS au ADDONS na utoe extensions zote usizozitambua au kama hujui Google hilo jina kabla ya kuitoa.


BAADHI YA MALWARE/ADWARE..
Ge Force (Browser extension)
YT downloader (Program)
Sense (Adware extenssion)


Download Tool ya kuwatoa hawa wadudu hapa AdWCleaner
 
Back
Top Bottom