DOKEZO Malipo ya maegesho ya SGR kwanini yasilipwe kwa control number? Huu mradi una mkono wa nani?

DOKEZO Malipo ya maegesho ya SGR kwanini yasilipwe kwa control number? Huu mradi una mkono wa nani?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Nimekuwa nikijiuliza maswali kuhusu utaratibu wa maegesho ya SGR kwenye stations zote kama mapato yatokanayo na ada ya maegesho yanaenda wapi?

Kama ni mapato ya serikali kwanini yasilipwe kwa control number? Mbona bookings za tickets za SGR zina control number lakini malipo ya maegesho unalazimika kulipa cash?

Tena utaratibu wa malipo sio rafiki inabidi uende dirishani upange foleni kulipia na kwenye pick hours mtu unaweza poteza 5-10 minutes unnecessary!

Kama tickets zina weza kuwa scanned hata kama ipo kwenye simu kwanini mteja wa TRC ashindwe kuscan malipo ya maegesho anapo toka?

Kweli kwa dunia ya sasa makusanyo yanafanyika kwa kupokea cash?

Ikiwa TAMISEMI wanalipisha parking fees kwa control number tena malipo ya Tsh 300 kwanini TRC inakusanya pesa mkononi?

Mradi wa SGR ni mikopo ya matrilion ya pesa sioni seriousness kwenye makusanyo kupitia mradi huu!

Mfano kwanini hizi stations chache za SGR zisi collaborate na Tanzania Postal Services watu wakatuma parcels ndogo ndogo zisizo zidi kilo moja kwa kuanzia. Kweli TRC na Posta wanashindwa kusafirisha documents from Dar to Dodoma and Dodoma to Dar?
 
Dah, hii nchi inaliwa kila sehemu, pesa zisizolipwa kwa mfumo maalum wa malipo ya Serikali lazima kuwe na upigaji.
 
Back
Top Bottom