Malipo ya fao la kujitoa NSSF

Malipo ya fao la kujitoa NSSF

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,265
Reaction score
4,452
Habari za leo;
Baada ya nenda uje na vuta nikuvute nyingi hatimaye nimefanikiwa rasmi kufungua madai ya fao la kujitoa pale NSSF ILALA.

Kilichonifanya nilete uzi huu hapa ni namna na jinsi nilivyopata usumbufu mwingi wa nenda uje hali ambayo imenifanya niulize wadau ili nijiandae kisaikolojia kuhusiana na tarehe ambayo nitapata malipo hayo.

Kwa mujibu wa muhudumu ambaye amenifungulia madai amenipa reference namba na kuniambia kuwa nirudi baada ya 90 days.Kwanza nimeshtuka nikasema kwa nini ila hakunipa jibu zaidi ya kuita anayefuata kwenye foleni

Sasa wadau kwa wale ambao waliwahi fikia hatua ya kufungua madai Je walifanikiwa kulipwa hasa ndani ya hizo siku tisini?na je kama ilichelewa sababu ilikuwa ni nini?Na je wanakujulisha malipo yako yanapokuwa tayari?

Nitashukuru kwa majibu mazuri

Mdau wangu
 
Kama ulifukuzwa kazi sahau ila kama ulufukuzwa utapewa .kukuambia uje ni kawaida yao kukuandaa kisaikolojia ila kukupa itajambo lingine
 
Mkuu fao la kujitoa lilishafutwa. Hautalipwa hiyo pesa mkuu. Utazungushwa tu
 
Mkuu fao la kujitoa lilishafutwa. Hautalipwa hiyo pesa mkuu. Utazungushwa tu
Mkuu nimeshafungua official claims ina maana bado watanizungusha tu au maana sijaelewa
 
Kama ulifukuzwa kazi sahau ila kama ulufukuzwa utapewa .kukuambia uje ni kawaida yao kukuandaa kisaikolojia ila kukupa itajambo lingine
.....unasomeka kweli !?
 
Mkuu nimeshafungua official claims ina maana bado watanizungusha tu au maana sijaelewa
Mkuu,usipoteze muda wako bure.
Mwezi wa tatu ndio bunge linakaa kujadili watu walipwe au wasilipwe,na kama ni kulipwa ni kwa njia gani.

Kwa sasa subiri hadi miezi 6 iishe ndipo uraise claims zako.

Hakuna cha 90 days hapo.
 
Mkuu nimeshafungua official claims ina maana bado watanizungusha tu au maana sijaelewa
mkuu kuna mtu namfahamu alifungua toka mwaka jana NSSF hadi leo ana miezi 9 kila akienda kalenda, nadhani wanavuta tu muda ifike sheria ipingwe nyundo kabisa, mwenyewe nilikuwa PSPF nimeshasahau kabisa.
 
KWA NYIE WAJUZI WA MAMBO NAOMBA KUHUSU HILI PIA MNIFAHAMISHE MIMI NI MWANACHAMA.WA LAPF NA KILA MWEZI WANAKATA KIASI CHA PESA KWENDA KWAO KWA MALIPO YA BAADAE SASA KWA UPEPO HUU ULIVYO NAONA KABISA NI HERI NIKAANDAA MAZINGIRA YA KUWEZA KUKIMEGA ATA HIKO KIDOGO NACHOJILIMBIKIZIA HUKO SASA SWALI LANGU NI JE WANAWEZA NIPATIA MKOPO KISHA WAO WAKAWA WANAKATA KIASI CHA PESA KUTOKA KATIKA ZILE ASILIMIA WANAZOKATA KILA SIKU NA SI HUKU TAKE HOME
 
NSSF imekwisha kutapeli tayari. Hao ni wezi, dalili za mwizi ni kukupatia ahadi ambazo hana uhakika nazo....miezi 3 ya nini??? Pesa ilikuwa yako tena walikuwa wanakukata bila kukupa taarifa. Wezi hao!!.... Pambana na wezi hao mkuu, pole sana!!
 
Mkuu nimeshafungua official claims ina maana bado watanizungusha tu au maana sijaelewa
Mkuu kwa jinsi nilivyofatilia taarifa za hili fao since early last year (personal follow up ya conversations mbalimbali), ni kwamba hii kitu hawatoi tena, nilimwuliza jamaa mmoja wa nssf akaniambia hiyo kitu haipo tena na hata ukistaafu unapewa amount ndogo tu ya mkupuo (3 months gross) then utapewa ndo ndo ndo 80% ya salary mpaka ukifa itastop, kwahiyo mkuu, ikifika siku nenda, al muhimu jiandae kisaikolojia
 
Hata kama umefungua mkuu, wamekufungulisha tu ili kupunguza makelele. Hawalipi siku hizi hii kitu
Mkuu cdhani kama wanalipa tena, mie nilifika ofsini kwao wakaniambia mpaka wapewe go on ya kutoa kwasasa imesitishwa. Kwahiyo mpaka ustaafu, na ukistaafu hupewi yote, unapewa 3Xgross salary then wanakupa kidogo kidogo kama pension
 
Mkuu kwa jinsi nilivyofatilia taarifa za hili fao since early last year (personal follow up ya conversations mbalimbali), ni kwamba hii kitu hawatoi tena, nilimwuliza jamaa mmoja wa nssf akaniambia hiyo kitu haipo tena na hata ukistaafu unapewa amount ndogo tu ya mkupuo (3 months gross) then utapewa ndo ndo ndo 80% ya salary mpaka ukifa itastop, kwahiyo mkuu, ikifika siku nenda, al muhimu jiandae kisaikolojia
Twafaa Kazi nifanye mie pesa achukue yeye tena kwa nguvu.
 
Mkuu cdhani kama wanalipa tena, mie nilifika ofsini kwao wakaniambia mpaka wapewe go on ya kutoa kwasasa imesitishwa. Kwahiyo mpaka ustaafu, na ukistaafu hupewi yote, unapewa 3Xgross salary then wanakupa kidogo kidogo kama pension

Mafao ya NSSF yaliyo chini ya 15mil kama sikosei unalipwa ndani ya 30 days kwa sababu yana kuwa processed kwenye Branch husika,ila Zaidi ya hapo mpaka yawe approved Head office ndio maana ya hizo 90 days.

changamoto iliyo mbele yako ni kwamba walisitisha kutoa hiyo ya Fao la kujitoa pending to sheria mpya inayokuja.Sheria mpya inayokuja nadhani inaweza pitishwa bunge la January hii.
Sijaipata ila kwa fununu ni kwamba unalipwa ka 38% at a go then nyingine kidogo kidogo mpaka pale utakapotwaliwa na bwana.
 
Ndugu yangu nashukuru kwa hili jibu lako,ila nilitaka kufahamu zaidi kwa wale ambao walishafungua madai maana mimi yangu nilitarajia ningelipwa ndani ya mwezi lakini sasa nimeambiwa miezi mitatu.Je kuna mtu humu ambaye alishafanikiwa kufungua na kulipwa ndani ya huo mwezi mmoja?
 
Back
Top Bottom