KICHINJIO 15
JF-Expert Member
- Oct 6, 2015
- 823
- 628
Habari za wikendi wanajamvi!
Kuna mkasa nilisimuliwa na nikaona siwezi kubaki nao moyoni mwangu bila kukushirikisheni wenzangu. Jaribu kwenda nami katika mkasa huu.
" Kuna mume aliyeishi na mkewe kwa miaka kama kadhaa baada ya kufunga ndoa ya Kiislamu. Mungu akawajalia watoto watatu. Mtoto wa kwanza ni wa kike ana miaka 11, wa pili wa kiume ambaye ana miaka 9 na wa tatu ni wakiume pia mwenye miaka 6. Tatizo lake alizaliwa na ulemavu wa akili.
"Matatizo ndani ya ndoa yalianza alipozaliwa mtoto huyu wa tatu. Niaka takribani 6 toka mifarakano ianze. Mume alianza kumtukana na kumpiga mkewe akidai kuwa amemzalia mtoto mwenye ulemavu wa akili. Akadai kuwa huyo mkewe ana laana ya ukoo ndo maana amepata mtoto huyo. Ndugu wa upande wa mume walimshambulia kwa matusi na masimango. Hali ikawa mbaya sana mle ndani lakini mke alivumilia yote hayo na kubaki ktk ndoa ili amlee mwanae huyo kipenzi.
Baadaye yule mume akaamua kumwachia nyumba yule mama na watoto wote watatu. Yeye akaoa binti kigoli na kuishi naye kwingine na wala hakutaka kujua kinachojiri kwa mkewe wa kwanza na watoto.
"Mkewe mpya akapata mimba. Muda wa kujifungua ulipofika akajipatia mtoto wa kiume, lakini mwenye ulemavu wa akili. Mtoto anatoa udenda muda wote. Yule baba akawa kachanganyikiwa na kuhusisha ulemavu huo na iman za kishirikina. Lakini akajipa moyo. Maisha yakaendelea.
"Baada ya miaka mitatu, mkewe huyo mdogo akabeba mimba tena. Alipojifungua, akapata mtoto wa kike. Huyu akawa na kichwa kikubwa kiasi kwamba shingo ikawa haiwezi kukibeba kichwa kile na kusababisha shingo iwe inakwenda upande. Muda mwingi mtoto alikuwa amelala. Udenda, kama ilivyo ada haukuisha mdomoni.
"Hali hii ikawafanya jamaa, ndugu na marafiki wa huyu mume wamshauri amrudie yule mkewe wa kwanza na kumwomba msamaha. Akafanya hivyo.
"Kwa hiyo sasa anaishi na wake wawili watoto watano, watoto watatu wakiwa na ulemavu wa akili. Watoto hao kwa sasa wanalelewa kwenye kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa akili."
Huo ndo mkasa niliosimuilwa. Napenda kushauri yafuatayo:
Tusiwe wepesi wa kuwalaumu wake zetu kwa ulemavu wanaozaliwa nao watoto wetu. Tujaribu kuangalia chanzo cha tatizo.
Aidha, tusiwanyanyapae na kuwabagua watoto hao kwani hawakuchagua kuzaliwa hivyo.
Tukiwafanyia mabaya, malipo yataanzia hapa hapa dunia.
Mungu akulindeni.