Malinzi, wafanyakazi wako tumewachoka kwa kuwa ombaomba

aka2030

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
2,657
3,679
Yamkini hali si shwari kwa wafanyakazi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) makao makuu yaliyopo Karume, kufuatia kudai mishahara yao ya miezi miwili na nusu.

Tangu kuingia madarakani kwa Jamal Malinzi hali ya taasisi hiyo imekua mbaya kila kukicha mpaka kupelekea kushindwa kuwalipa mishahara watumishi wa taasisi stahiki zao tokea mwezi Machi, 2016.

Habari za ndani zinasema hiyo imetokana na Malinzi kuwa na matumizi ya ufujaji wa pesa za TFF kwa maslahi yake binafsi, kwani yeye ndio anapanga matumizi ya taasisi hiyo kwa kutazama sehemu alizo na masilahi nayo, huku akiwaacha wafanyakazi wakiungua na jua.

Suala hili linaonekana kuwa sugu, wafanyakazi hawajalipwa mishahara ya mwezi Machi, Aprili na sasa ni katikati ya mwezi Mei, na hakuna taarifa wala dalili ya kupata mishahara yao hivi karibuni.

Rai kwa serikali, PCCB, wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo naombeni mfuatilie na kuichunguza hii taasisi muhimu nchini kwa kuwa na matumizi ya kufuja hela na kutowathamini watumishi wake.

Mfanyakazi ambaye hajalipwa mishahara yake kwa miezi mitatu, unategemea anaishije? Hapo ndio chanzo cha kuomba rushwa kwa viongozi wa vilabu?
Kwa nini kipindi cha Malinzi hali imekua tete TFF kifedha tofauti na utawala wa Tenga? Tenga aliwathamini wafanyakazi wake kwanza , huku Malinzi akiwathamini marafiki zake.

Wafanyakazi wako wamezidi kutuomba hela mitaani wengine tunawadai madeni makubwa mpaka sasa au wataka tuwaaibishe? Baba uwe na aibu.
 
Yalifanyila makosa makubwa sana kumchagua Malinzi hapo TFF......huyo si mdau wala mpenzi wa soka bali ni mtu wa maslahi......tangu ameingia yeye hapo TFF imekuwa ya hovyo sana.....maslahi yamewekwa mbele kuliko soka.....ligi imekosa mvuto na kuwa ya timu moja yenye tuhuma za kununa mechi ili itwae ubingwa......
Marefa wanafanya maamuzi mabovu kwa ajili ya kuibeba timu fulani lakini hawachukuliwi hatua badala yake wapenzi na mashabiki wa soka wanaamua kujichukulia sheria mikononi kwa kuwapopoa mawe......
 
ma mods wa jf nao nikisema ukweli kuhus hutu bwana thread zangu wanaziedit zingne wanaxitoa siwaelew
 
Hapo mimi ndiyo wananichosha
Wamekuwa kama mawaziri wa magu nao hawa mods wa jf

Nazani watofautishe mpira na mambo ya siasa mpira wetu unafaa tupiganie kisawasawa bila kumuogopa mtu yoyote yule ile mradi mtu awe na ukweli na kile asemacho
 
mada ya mpira wameipeleka jukwaa la elimu
 
Mi nadhani huyu mheshimiwa na uongozi wake hapo TFF kwa ujumla ni wa hovyo Sana, kumekuwa na maamuzi ambayo ni blunders Sana hali ya kiuchumi ya taasisi imekuwa ni mbaya tangu kuingia kwake, upangaji matokeo, ratiba ligi kubadilishwa pasipo na sababu za maana baadhi ya timu kuwa na nguvu, upendeleo kuliko hata hiyo TFF yenyewe. Huyu Jamali malinzi hiyo sehemu yupo kimakosa na anapaswa atoke tu.
 
Lilikuwa kosa kubwa sana kumchagua Jamal, Ile move ya kwanza kumuondoa ndio ilikuwa sahihi, vinginevyo hamna Mpira wala nini, kitendo cha TFF Kuhamisha ofisi Karume ni kuongeza gharama japo sina hakika kama ofisi imerudi karume.
 
Kabisa Mkuu! Jamaa kuutaka uraisi wa TFF ulikuwa wa maslahi binafsi, more like to clear his conscious na yeye aonekane wa maana. Inasemekana kule Cargo stars hakuwa na mamlaka kivileee; Big Brother (Dionis) ndio kila kitu.
 
atoke tumemchokaaaa
 
Lilikuwa kosa kubwa sana kumchagua Jamal, Ile move ya kwanza kumuondoa ndio ilikuwa sahihi, vinginevyo hamna Mpira wala nini, kitendo cha TFF Kuhamisha ofisi Karume ni kuongeza gharama japo sina hakika kama ofisi imerudi karume.
Lakini naona kama TAKUKURU wanamlinda sana. Hivi tangu watuambie wanaifuatilia TFF mpaka leo hatuoni lolote na bado anapeta. Au huo uchunguzi hauna mwisho? Kila siku hawa jamaa wa TAKUKURU wanasema tunaendelea na uchunguzi au wanafikiri tusahau ili wayafute madhambi kimya kimya?
 
Lakini hata mtendaji wake mkuu anamshauri nn malinzi maana hata yeye ukiona nikama yupoyupo tu tangia akiwa enzi za kandambili hakuonyesha vision yoyote.
 
Lakini naona kama TAKUKURU wanamlinda sana. Hivi tangu watuambie wanaifuatilia TFF mpaka leo hatuoni lolote na bado anapeta. Au huo uchunguzi hauna mwisho? Kila siku hawa jamaa wa TAKUKURU wanasema tunaendelea na uchunguzi au wanafikiri tusahau ili wayafute madhambi kimya kimya?
MALINZI NI JIPU TFF.
 
Back
Top Bottom