gollocko
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 2,945
- 2,281
Hivi wanaJF hebu mnijuze, pale wizara ya maliasili na utalii kuna nini? Maana kila kiongozi anaeteuliwa huwa hafai na mwishowe huondoka kwa kashfa; kwa kuthibitisha hili hebu tujikimbushe hawa wafuatao:
1. Zhakia Megji – Huyu alituhumiwa kwa kjimilikisha vitalu vya uwindaji isivyo halali
2. Prof. Jumanne Maghembe – Yeye alituhumiwa kufanya mabadiliko makubwa ya wakurugenzi na makamishna pale wizarani kwa utashi wake pia alipandisha bei ya vitalu na wanyama isivyo kawaida.
3. Antony Dialo na Saleh Pamba- Hawa walituhumiwa kwa kufanya biashara ya magogo nje ya nchi ilihali ikiwa imepigwa marufuku na serikali.
4. Shamsa Mwangunga - Yeye na katibu wake Blandina Nyoni walikuwa hawaelewani kabisa kiasi cha kila mmoja kufanyia kazi za serikali nyumbani kisa ni Mwangunga kutuhumiwa kutorosha magogo nje ya nchi bila vibali.
5. Ezekiel Maige- Huyu ndio balaa, licha ya kutuhumiwa kugawa vitalu kwa rushwa na kuwa na ukwasi wa kutisha bado katika kipindi chake wanyama wametoroshwa nje ya nchi huku yeye akijifanya hajui kinachoendelea.
Hapa ndo najiuliza hapa maliasili na utalii kuna nini? Mbona kila anayepelekwa mambo huaribika?