Sophist
Platinum Member
- Mar 26, 2009
- 4,486
- 3,407
Sasa ni dhahiri kuwa Rais wa nchi analipwa shilingi milioni tisa na laki tano (9,550,000.00). Rais ametamka na CAG mstaafu akathibitisha hivyo.
Tukichukua kigezo cha mali alizokuwa nazo Mwl. Nyerere na hata Ndugu Mwinyi (ingawa kulikuwa na issues za Sea Cliff na nyinginezo) mara baada ya kumaliza muda wao wa uongozi, tunathibitisha kuwa Rais wa Tanzania hakuwahi kulipwa mshahara mkubwa.
Lakini kuna marais wastaafu Mkapa na Kikwete waliomaliza muda wao wa utumishi wakiwa na mali nyingi, kwenye mitaji na real estates (miliki za Ardhi na majumba).
Hebu tutathmini gharama zilizojenga/thamani ya miliki zilizopo Msoga au Lushoto, Dar es Salaam (Sea View, Mbezi, Masaki, Regent Estate, Mikocheni na kadhalika), tulinganishe na mishahara ya miaka 10 kwa Mkapa na Kikwete halafu tuwaulize; ziada nje ya malipo rasmi ya mishahara yao ilitoka wapi? Ni vyanzo halali?
Tusiwadhalilishe wala kuwakejeli, ila tuwahoji kwa adabu kwa lengo la kuhakikisha uwazi na uwajibikaji unaleta manufaa nchini Tanzania.
Tumeanza kujenga Tanzania isiyokuwa na rushwa chini ya Serikali/uongozi wa JPM.
Ni hayo tu.