BOB LUSE
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 3,738
- 3,198
I greet you my elders,
Mali naongelea neema katika familia ambayo inawapa nafasi ya kumudu mahitaji yao ya chakula na maendeleo.
Familia ikipata neema ya kupata mali baadhi ya ndoa zingine zinapitia misukosuko mpaka kusambalatika.Mali badala ya kuwa baraka, inakuwa mtego wa kuangamiza familia zilizokuwa zimeshikamana na kuelewana.
Baadhi ya mambo yanayochangia hali hiyo ni kama ifuatavyo.
1) Kuna kuwa hakuna maandalizi ya kisaikolojia ya kutosha vichwani mwa wanandoa kuumiliki utajiri wanaoupata kwa mipango thabiti ya pamoja ya wanandoa,kwakuwa hela zingine zinapatikana kwa njia za mkato bila kuzitarajia.(deal)
2) Mwanamke kutaka kumdhibiti mume kwa kuwa katika jamii imejengeka kuwa mwanaume akipata hela umeshampoteza, mwanamke anatumia njia zozote atakazoona zinafaa kumthibiti mume, ikiwezekana anataka awe kichwa cha familia,hapa panaleta cheche.
3) Mwanaume kutaka afanye mambo kimyakimya kwani naye mtaani kwake kaambiwa sio kila kitu umweleze mkeo mengine fanya asijue!Pia hapa panaleta patashika
4) Ndugu lawama,kuna ndugu wengine wanapenda washirikishwe pia wanufaikekatika hizo mali,ikiwa mwanaume/mke atashindwa kuwamudu ndugu zake hiyo ndoa italeta figisufigisu.
5) Kutomshirikisha Mungu katika mipango ya hiyo mihela!.Mungu anapowapatia utajiri (kwa waamini, Mungu ndiye atupaye utajiri sio akili zetu) anakuwa na makusudi,hivyo lazima mali yenu ionyeshe utukufu wa Mungu na kusimama kwa nafasi katika kusudi ulilopewa ukijifanya hela zako, lazima ufurahie na familia isambaratike.
Nakaribisha mwenye mchango tofauti tuboreshe familia zetu ili tufaidi mali na kuwaachia wana wa wanetu urithi.