MALEZI YA WATOTO NA MATOKEO YAKE

MALEZI YA WATOTO NA MATOKEO YAKE

Tan1947

Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
40
Reaction score
42
Heshima kubwa iwe kwenu wadau wa jukwaa hili.

Yapo baadhi ya mambo ambayo ningependa tushirikishane wadau.

Katika maisha yetu ya kila Sisi kama wanadamu wapo baadhi ya watu waliobahatika kupata familia na katika familia zao Mwenyezi MUNGU akawajalia kupata watoto pamoja na Kuwa na maisha bora Kwa kila mtu Kwa kiasi chake.

Leo ningependa kuyaangazia Mahusiano baina ya wazazi na watoto wao katika familia zetu za kisasa{Naziita za kisasa Kwa muktadha wa malezi yenye mrengo wa kimagharibi}.Katika Maisha ya familia zetu nyingi wapo baadhi ya watu walioajiri wasaidizi wa kazi za ndani{House maids/Girls} ambao huwa wanawalipa Kwa kila mwezi.

Kutokana na uwepo wa house girls wapo wazazi ambao huwakataza watoto wao kufanya kazi yoyote Ile nyumbani.Yumkini kutandika kitanda,kuosha vyombo ama kufua nguo. Hali hii huwa wanaifanya wakihisi ni jukumu kuu la ma house girls hao eti vile wanawalipa mishahara.

MATOKEO YAKE;
katika kundi kubwa la vijana wengi waliolelewa katika mazingira hayo kumekuwa na vijana wasioweza kujisimamia Kwa lolote. Kwa mfano, sasa hivi sio ajabu kumkuta binti wa kike mtu mzima asiyejua kupika,kufua ama kujisimamia kimaisha{Naposema kujisimamia namaanisha uwezo wa kujiongoza bila kutafuta usaidizi}.
Yumkini wapo wanaume wengi wanaoshindwa kuoa/Na walio oa mabinti wasio weza kupika,upo mfano mmoja kuna jamaa alioa mke ambaye alikuwa anapitia msosi take away kila akitoka kazini,yaani jamaa anatoka kazini anakuta chakula cha usiku ni kuku robo na chips na soda.

Vivyo Leo hii kuna wanaume ambao hawajui kufua,yaani unakutana na mtoto wa kiume anamkodisha mtu amsaidie kufua nguo zake mpaka nguo zake za ndani.Wapo wanawake wanalalamika kudate na mwanaume ambaye hawezi kujisimamia{kukitokea changamoto ama shida yoyote lazima aseme Kwa mama yake }wengine hawawezi hata kupika{kiuhalisia mwanaume anapaswa kujua kupika japo vyakula vya msingi kama wali/ugali}. Kuna watoto wa kiume wengine Kwa kuzoea kufanyiwa kila kitu wamekuwa waoga hata wa kujitegemea Kwa kuishi wenyewe yaani mtu amesomeshwa,ana kazi na bado anakomaa kuishi home.Wapo pia wenye kazi na bado wazazi wao ndio huwalipia kodi

Sasa hivi sio ajabu kukutana na MTU kahitimu kidato cha sita lakini hawezi kuapply vyuo mpaka asaidiwe.

WITO
Wazazi waleeni watoto wenu mkiiwaza kesho yao. Mnawatengenezea matatizo
 
Ngoja nisome kwa makini
 
Malezi yamekuwa magumu sana

Primary source inaweza Kuwa njema lakini vipi kwa upande wa secondary..
 
Watoto wamekuwa mdebwedo ,anahitimu elimu ya msingi hata kufua kichupi/ boxer anachovaa hajui wala hawezi ndio sababu mapunga yanaongezeka siku hadi siku
 
Kweli kabisa na ndoa nyingi zinaharibikia kwenye malezi. Watoto wengi wamelelewa malezi sio bora ndio wanayaishi mpaka ndoani. Ndio maana ndoa siku hizi hazidumu. Elimu ya malezi kwa.Wazazi inatakiwa itolewe kwa kiwango cha juu.naona wapo watumishi mbali mbali wanaojaribu kuzungumzia sana suala malezi. Wazazi wafuatilie wajifunze
 
Back
Top Bottom