Display Name
JF-Expert Member
- Feb 11, 2014
- 423
- 451
Salamu wakuu,
Maendeleo ya teknolojia yana changamoto zake na pia faida kubwa sana kwenye maisha yetu, hii pia imeonekana kwenye malezi ya watoto na maisha yao kwa ujumla
Je, watoto wanaolelewa kwenye kizazi hiki cha kununua vitu vya kuchezea kimepoteza ubunifu ukilinganisha na kizazi ambacho watoto walikuwa wanatengeneza vitu vya kuchezea wenyewe?
Hapo zamani kidogo mtoto akitaka kucheza mpira itampasa atengeneze mpira mwenyewe kwa vifaa vilivyokuwa vinapatikana kama vile nguo chakavu, vipande vipande vya magodoro na kamba, lakini sasa hivi mtoto huomba anunuliwe mpira dukani
Vile vile, mtoto akitaka mdoli wa kuchezea ilimbidi achukue nguo chakavu na kutengeneza mdoli wake au wenginge walitengeneza kwa kutumia mkungu wa ndizi ila kwa sasa mdoli anapatikana dukani
-
Pia, miaka ya nyuma kidogo watoto walikuwa wakitengeneza magari ya aina tofauti tofauti kwa kutumia makopo au nyaya, kamera kwa kutumia vikopo vilivyoisha mafuta ya kujipaka na hata nyumba ya kutumia maboksi.
Njia hii iliwafanya watoto wa miaka hiyo kuwa wabunifu na wenye kufikiria kwenye sanaa ukiwalinganisha na watoto wanaonunuliwa kila kitu kikiwa kimetengenezwa.
Je, wewe una maoni gani kwenye ukuaji wa teknolojia na mabadiliko haya? Unadhani watoto wa sasa wanapoteza uwezo wa kuwa wabunifu ukilinganisha na miaka ya nyuma?