The secretary
JF-Expert Member
- Jan 14, 2012
- 4,148
- 2,542
huo ndo ujinga wa wazazi wengi wanaoelekeza akili zao katika kusako shekeli halafu wanasahu kama wanawatoto home
usilete za uswazi, acha familia zijilee, we utamtafutia msichana mwingine?
lea familia yako, achana na familia za watu
Mueleze bana!!! kabla hali haijawa mbaya zaidi...Huo ndio tunaita ujirani mwema...Ingekuwa ni mwanao anatendewa hivyo ungependa jirani akutaarifu kinachojiri unapokuwa hauko nyumbani...ukija kusikia huyo mtoto amefariki labda kwa mateso ayapatayo kwa huyo binti utajilaumu sana.
YAANI!
iKO TRICKY LAKINI.
Kuna watu ukiwaambia wanasema unawachonganisha na wafanyakazi wao.
Iliwahi kuntokea nikajiskia vbaya sana.DADA wa jirani alikua anamtesa mtoto - anampiga, anamwacha na wahuni kijiweni kisha yeye anaenda zake kuzurula. Nikachukua jukumu kwaarifu wenye mtoto.Jibu walilonipa nilichoka.
"Huyo dada anamwacha mtoto hapo ili kwenda kuchukua maziwa, hivyo siyo vibaya." Hawakujali hata kama kwa kumwacha kijiweni masaa 4- 6 ni hatari kwa mtoto.Mtoto angenajisiwa na wavuta bangi? Hayo ni maziwa gani yanachukuliwa kwa masaa? Na je huko kumpiga mtoto kila mara nako kulikua na sababu? Nilijiskia vibaya ile mbaya! Nikakoma kuingilia maisha nyumba za watu!
Mwambie bwana huwezi utaokoa maish ya huyo mtoto kunyweshwa uji naman kuna mtoto alikufa hivi hivi nakwambia. Tafadhal sana. Wambie hata ingekua ni mimi mama wa mtoto ningependa niambiweNna jirani yangu mwenye mtoto wa mwaka mmoja. Ye na mume wake wote wameajiriwa kwahiyo huwa wanamuacha mtoto na dada wa kazi.
Kitu cha kwanza kunotice ni kwamba siku mmoja wao akiwepo nyumbani mtoto halii lii sana.Mpaka kuna wakati hua nadhani labda wametoka kwa ukimya kumbe wapo. Ila wakiwa hawapo mtoto analia kila saa, na dada wa kazi full kumfokea na kumtisha kumpiga(pengine hua anafanya kweli).
Sasa juzi ndio alinichosha kabisa. Nilimkuta kakaa barazani alafu kamlaza yule mtoto juu ya miguu yake, kichwa kimegusa sakafu alafu anamnywesha uji. Uji mwingi unaishia chini na puani, mtoto analia, dada ni kelele tu "ntakupiga!!!"kwa wingi na kulalama kuhusu uji unaomwagika.
Sikusema neno ila leo nimefikiria weee nikaona kuwa mimi nisingependa mtoto wangu awe analishwa kwa style hiyo au kupigwa hata kufinywa na mtu yeyote yule katika umri huo. Sasa najiuliza kama nimweleze jirani namna mwanawe anavyokuwa treated akiwa hayupo au la. Kama jibu ni ndio, nianzeje????
Maoni tafadhali.
hivi we ulishapaona labour nahisi una roho za huyo dada