#Malezi - Maadili ya mtoto ndani ya familia na jamii ni jukumu la nani?

Sema Tanzania

JF-Expert Member
May 18, 2016
251
465
Katika safu hii ya malezi leo tunaangazia suala zima la kuporomoka kwa maadili ya mtoto ndani ya familia na kwenye jamii.

Mara nyingi jamii ya Tanzania imekuwa ikimtupia lawama nyingi sana mzazi wa kike, yaani mama, kwamba ndiye chanzo cha kuporomoka kwa maadili ya mtoto ndani ya familia na jamii kwa ujumla. Hii ni kwa sababu mama huwa karibu zaidi na mtoto tangu mtoto anazaliwa, anatambaa, mpaka anapofikia hatua ya kuongea. Hatua hizo ni juhudi kubwa zilizofanywa na mama, lakini pia tukigeukia kwa upande mwingine wa mzazi wa kiume, yaani baba, anatakiwa kuwa sehemu ya malezi. Kwa kuwa mtoto aliyezaliwa ni wa wazazi wote wawili na si wa mama peke yake.

Baba anatakiwa kushirikiana na mama kumlea mtoto katika hatua zote muhimu za ukuaji wake kwa kumpatia huduma stahiki kama vile chakula, mavazi, elimu na matibabu lakini vilevile kwa kutenga muda wa kukaa na kumlea mwanae. Kutokuwepo kwa ushiriki wa baba katika malezi ya mtoto kunamfanya mtoto azoee mazingira ya malezi ya mama pekee kwani baba hatengi muda maalum wa kukaa na kuzungumza na mtoto ili kufahamu mahitaji, tabia pamoja na mwenendo wa mtoto.

Ifahamike kwamba mtoto huanza kujifunza maadili kuanzia ngazi ya familia, yaani kutoka kwa wazazi au walezi wake kwani hao ndio watu wanaomzunguka kwa karibu zaidi. Halafu baadae huendelea kujifunza maadili kutoka sehemu mbalimbali kama vile shuleni na kwenye nyumba za ibada.

Hivyo basi, ikiwa mzazi au mlezi atakuwa anafanya mambo ambayo ni kinyume kabisa na maadili mema kwenye familia au jamii kama vile ulevi na kuwepo kwa mgogoro wa kifamilia mpaka kufikia hatua ya kugombana, kupigana ama kutukanana mbele ya mtoto, basi atambue kuwa mtoto ataiga kutoka kwake na athari kubwa itakuwa kwa mtoto. Huo ndio utakuwa mwanzo wa kuporomoka kwa maadili ya mtoto ndani ya famillia na kwenye jamii.

Jamii ifikie mahali ambapo itaweza kubadili mtazamo wake katika kutupia lawama upande mmoja wa familia, yaani kwa baba au mama kuwa ndiye muhusika mkuu katika kuporomoka kwa maadili ya mtoto ndani ya familia na jamii. Kwani wazazi au walezi wote wawili wana wajibu wa kumlea mtoto na kumpa matunzo, ulinzi na malezi mazuri kwa usalama wake ili kujenga jamii yenye watu wenye maadili mema.

Tabia aliyonayo mtoto wako inatokana malezi anayopewa kutoka kwa wazazi au walezi wake tangu anazaliwa hadi anakua mtu mzima. Ikiwa mzazi au mlezi hatachukua jukumu la kumuonya au kumfundisha mtoto maadili mema, basi ataendelea na tabia hiyo mpaka kufikia ujana na hatimaye uzee wake. Jamii inahitaji mafunzo na elimu ya kutosha kuhusu malezi ya mtoto, ambapo mafunzo na elimu hii hupatikana kutoka katika taasisi mbalimbali nchini na kwa namna mbalimbali mfano makala hizi za malezi.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia kurasa zetu wa Facebook, Instagram na JamiiForums: Sema Tanzania; Twitter: @SemaTanzania na www.sematanzania.org. It's Possible|Inawezekana!
 
Makosa yanaanza kabla mtoto hajazaliwa... ni asilimia ndogo sana ya Watanzania huwa wanafanya maandalizi kabla ya kuamua kuzaa watoto. Kwa hiyo, unaongelea familia ambazo watoto wamepatikana kwa 'bahati mbaya' - hakuna maandalizi yaliyofanyika. Ukijumlisha na ukosefu wa ajira, uzazi katika umri mdogo na tamaduni zetu ... ni akina baba wachache sana wanaweza kuhusika na malezi ya mtoto.

Mbaya zaidi, wengi wanaingia kwenye mahusiano wakiwa hawana malengo ya muda mrefu. Single mothers wanazidi kuongezeka. The problem is deep.
 
Swala la malezi ni la wazazi wote bila kubagua, mama anatakiwa awajue watoto lakini baba pia ikiwa yeye baba ndio msimamizi wa nyumba. Ni sawa na meneja mauzo (mama) wakati mkurugenzi mkuu wa kampuni (baba).

cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
cₐᵣₑₑₘ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿᴰ
 
...Swali..
Hii inakuaje pale baba anapokua mlevi..alaf akirudi ni matusi mwanzo mwisho huku akigombana na mama licha ya yote hayo..bado mtoto huyu w 15yrs anakua na maadili mazuri licha ya tabia za wazazi....je huyu mtoto tunamchukuliaje??..nini kimefanya mtoto huyu anakua na maadili mema huku wazazi wakiwa hawajitambui toka anazaliwa........
 
Intel5500,


Watoto wengine wanazaliwa tu ,,binadamu wazuri”, in sawa na kuna watu wanaamua kuwa wezi au makahaba ukiwauliza wanasema maisha magumu lkn wapo watu wanaopitia magumu maishani na hawawezi kuiba wala kufanya ukahaba.
 
Back
Top Bottom