Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Kuna nchi nyingi duniani ambazo viwango vya maisha ya wakazi havina tofauti na Tanzania, lakini zinaendesha mashirika ya ndege kwa ufanisi mkubwa sana. Imekuwa ni habari njema kwamba awamu ya tano inajipanga vyema ili ATCL iweze kuanza kufanya kazi kimataifa kwa kutegemea ndege kadhaa (inasemekana ni ndege nane).
Faida za wingi wa ndege zetu zitakazokuwa zikafanya safari katika nchi nyingi duniani, ni nyingi sana kiuchumi. Lakini kilichochangia kudumaza na kuua mashirika mengi ni ukosefu wa utashi wa kisiasa (political will). Unapokosekana utashi wa kisiasa, hata ile tabia ya kuiona mali ya nchi kama inao wajibu wa kutunzwa na kila mtu, na yenyewe inakosekana. Kunakuwepo na tabia ya kuingilia mambo yaliyopangwa kufanyika kitaalam. Wakurugenzi na mameneja wanajikuta hawapewi ule uhuru wa kutiririka kitaaluma, mwishowe wanakatishwa tamaa na kuamua kutafuta ajira nje ya nchi.
Ninaamini ndege nane zitakazoanza kama mtaji wa ATCL, zinaweza kununua ndege nyingine zaidi ya 20. Utashi wa kisiasa ukiwepo hata mashirika yote ambayo serikali ya awamu ya tano inayo nia ya kuyachukua tena, yataweza kuwa na mchango chanya katika ukuaji wa uchumi. Huu ni muda ambao wale wenye mamlaka serikalini, wanapaswa kujifunza kutokana na kushindwa kuleta ufanisi kiasi cha kufikia hatua ya kutelekeza mashirika na viwanda.
Utashi wa kisiasa ukiwepo na kupewa msisitizo naamini ATCL itakuwa ni mojawapo ya mashirika ya ndege yenye ubora mkubwa barani Afrika.