Kosa la kumchukua mwema ukamuweka ndani ya waovu ili akufumulie uovu,watakaomuona anaambatano na hao Waovu watamuhesabu ni muovu pia.Ni heri kumtumia mwovu kuangamiza waovu wenzie,kumtakasa mwema ambae ameshirikiana na waovu kwa nia ya kufumua uovu, kwa dunia ya kawaida ya walio wengi hawatakuelewa, kutaka mwema asieleweke ni muovu na mtu huyo akasimama kwenye Public inayotaka kuona Mwema ni Mwema na Muovu ni Muovu,ni kazi kubwa na mfumo huo kwa ulimwengu huu wa sasa mtu wa aina hiyo atakiwi kuwa ni mtu wa watu [Public Figure].
Na haikua sahihi kwa mwema kushirikiana na waovu, muache muovu amfichue muovu mwenzie,kisha wote wasukumiwe hukumu inayostahili wao kupewa.
JK leo hii katufikisha hapa hakika kuna mambo ambayo pia nae kama binadamu mwenye mapungufu kwa kuwa sio Mungu, angependa kuona yanakufa ama yanapotea kwa kuwa yalimkwaza hapo awari kabla ajawa Rais,hayo ni mapungufu ya kibinadamu, lakini ndani ya mapungufu hayo kumezaliwa jambo ambalo kwa namna fulani nimelipenda na ambalo kwa watu wengi wa PWANI wanalo KUCHUKULIA VITU MUHIMU KWA MZAA.[Si nzuri kwa Kiongozi mwenye vision] ila kwa mzaa huu wa kipwani Watanzania wamepata UHURU,ambao kwa KATIBA HII YA SASA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,ambayo inampa Rais Mamlaka makubwa. Kama KWELI bila UNAFIKI Rais Kikwete angesema atumie RUNGU hilo leo hii kusingekua EPA,KAGODA wala DOWANS nani asiyejua Mheshimiwa aliyepita alivyolitumia RUNGU hilo.Leo hii mengi tunayoangaika nayo ni yale awamu iliyopita ukichanganya na mengineyo mapya kama RICHMOND.
Mheshimiwa huyu katika hili la uhuru tulionao leo,anastahiki pongezi sana.kuna vigogo wenzie nahisi wanamuona kama legelege kwa kuwa akutumia mabavu [Dola] kuzibiti matukio yaliyojili.Kwani kuna kashifa ngapi zilikua zinajulikana zama hizo lakini kupitia uthibiti hakuna yoyete iliyofika kwa UMMA na kama ilifika nayo illikandamizwa na kupoteza uhalali wa kujadiliwa na UMMA kwa uwazi kama inavyotoke kwa sasa.
Mheshimiwa huyu kwa kusoma kwake alama za nyakati na kuchukua upepo acha mwenye ubunifu wake kumzidi mwingine kati [Mafisadi na UMMA] ambao kwa ngazi ya Urais ukivaa viatu vyake kwa Mujibu wa katiba yetu [Mfumo] wote ni wake.
Yaani Wananchi na Mafisadi [Sipendi kusikia kuwa RACHEL ndio mafisadi pekee, wakati kuna jamaa zetu kibao mitaani tunawajua ni Mafisadi, natulikua tunawashabikia kila siku kuwa niwajanja kitaa] wote kwa pamoja tunaunda Taifa la Tanzania,kwa mfumo wetu ulivyo na madaraka makubwa aliyonayo Rais, ukichukilia historia ya mfumo wetu wa kutawala Rais anadhamana ya mambo mengi sana kwa kila raia na maliasili zetu.Urais huo ukipata Rais mfujaji aina ya marehemu Mobutu na king'ang'anizi kama Mzee Mugabe nchi hii ni tofauti kabisa.
Kwa kuwa Rais anamamlaka [Invest] mengi na makubwa na ambayo yanategemea Utashi wake ama Hiari yake kuyatekeleza.Makosa yatakayotokea yanatokana na matumizi ya Utashi na Hiari yake na si kwa Muongozo wa Sheria mama. Makosa hayo ambayo yalitakiwa kudhibitiwa na Sheria Mama [KATIBA] yasitendeke yanatendeka au la UMMA usimamie kupingana na Sheria hiyo mama yasitendeke.
Mheshimiwa kwa hili alitumia Utashi wake na Hiari Yake lakini pia akauachia UMMA uamue lipi ni sahihi kwao na kwa faida yao, uku akiwa amewabeba wote kati ya Mafisadi na UMMA.Kwa kuwa vita hii ni dhidi ya mafisadi na wananchi, mshindi ni UMMA ambao kwa pamoja wanaunda jumuhiya na kundi kubwa lenye kudai haki.Na kwa kua mtoa haki anauwezo wa kubana ama kutoa basi kama akitoa haki hiyo anahitaji kupongezwa kwa kuwa ILITAKA MOYO KUFANIKISH HILO.