Malecela kumrudisha Sitta kwenye uspika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malecela kumrudisha Sitta kwenye uspika

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Jun 29, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Malecela kumrudisha Sitta kwenye uspika

  Bunge la Tanzania likiendelea na mikutano yake
  Kizito Noya, Dodoma na Boniface Meena Dar

  WAZIRI Mkuu mstaafu, John Malecela amesema atafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta anarudi katika uspika baada ya uchaguzi mkuu.Malecela alifanya kampeni hizo alipokuwa akichangia hotuba ya makadirio ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyowasilishwa bungeni jana na Waziri Profesa David Mwakyusa ambayo imetengewa Sh678,421,483,000.

  Malecela alisema atahakikisha Sitta anarudi kwenye uspika kutokana na utendaji mzuri wa kazi katika kuliongoza bunge tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo.


  “Mimi binafsi naomba dua ili urudi bungeni na ukifanikiwa, nitafanya kila ninaloweza kuhakikisha unakuwa spika tena ili tuendelea kupata utendaji wako uliotukuka,” alisema Malecela.

  Mbali na kumwombea Spika Sitta arudi Bungeni, Malecela alijipigia kampeni mwenyewe kwa kuwataka wapigakura wake wa jimbo la Mtera, wamchague tena ili aendeleze mema aliyoyaanza.

  Malecela aliwataka wapigakura hao kuwapuuza watu aliosema wanafika jimboni kwake na maneno yasiyo na maana yenye lengo la kutaka kumng’oa katika nafasi ya ubunge.

  “Jimboni kwangu Mtera, ninawaomba na kuwasihi wananchi wawapuuze hao wanaokuja na maneno ya hovyo hovyo. Msisikie maneno yao bali tuendelee kuwa pamoja ili tukamilishe malengo yetu,” alisema.

  Akizungumzia jimbo lake Malecela alisema kuwa serikali imefanya makubwa kwa kuboresha sekta ya afya, lakini aliiomba iongeze kasi katika kuboresha zaidi.

  Alisema katika kipindi chote cha uwakilishi bungeni jimbo la Mtera limepata mafanikio mengi ikiwamo ujenzi wa zahanati katika kila kijiji.

  Pia anamwombea kwa Mungu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aweze kurudi kwenye nafasi yake baada yauchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

  Awali, Malecela aliwatolea uvuvi wapinzani kwa kuhoji wanataka serikali iwafanyie nini wananchi ili waridhike, kama imefanya mambo ya maendeleo.

  Malecela alisema “Msituhukumu kwa hatua tuliyofikia bali tuhukumuni kwa tulikotoka,” alisema Malecela na kuongeza:

  “Tulipopata uhuru nchi hii ilikuwa na madaktari watatu tu, lakini leo tunashuhudia maendeleo yapo karibu katika nyanja zote. Bado wenzetu mnasema hatujafanya kitu. Mnataka Serikali iwabebe wananchi ndio mkubali imewafanya mambo ya maendeleo?” alihoji.

  “Mimi nausifu uongozi wa awamu ya nne na hasa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Naibu waziri Aisha Kigoda amekuwa akijibu maswali kama ya wizara kikamilifu! Mnataka mafanikio gani. Awamu ya nne ina maendeleo makubwa.” aliongeza.

  Malecela alisema hayo baada ya kambi ya upinzani katika hotuba yake ya makadirio ya matumizi ya bajeti hiyo kusema kimsingi serikali imeshindwa kufikia malengo yake, hasa katika wizara ya afya.

  Msemaji wa kambi hiyo Dk Ali Tarab Ali alitaja baadhi ya maeneo aliyoeleza kuwa hayajafanikiwa vizuri kuwa ni pamoja na wizara kutegemea wafadhili katika miradi yake kwa karibu asilimia 98 na kuendelea kutoa malipo mengi kwa wafanyakazi hewa.

  “Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inatekeleza wajibu wake wa kidemokrasia wa kutao maoni ili chama kinachotawala kiyafanyie kazi kwa maslahi ya Taifa. Sisi tnasubiri tupewe ridhaa na wananchi ili tutekeleze mipango hii ambayo wenzetu mmeshindwakutekeleza,” alisema Dk Tarab.

  Wakati akianza kuchangia hoja hiyo, Malecela alisema kuwa ni muhimu wapinzani wakaelewa kuwa CCM imefanya mambo mengi tokea uhuru hiyo ni muhimu wakaheshimu.

  "CCM itaendelea kuongoza kwa kishindo hivyo upinzani wakubali hali halisi. Chama (CCM) kimeitoa nchi mbali kuanzia uhuru wakati tukiwa na madaktari watatu na sasa tunao wengi hivyo serikali si ya kuhukumiwa kwa kuwa tulikotoka ni mbali,"alisema Malecela.

  Source: Mwananchi
   
 2. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tumewazoea hawa!!! Hivi miaka 37 haimtoshi huyu mzee?
   
 3. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  These are the leaders of our country!
   
 4. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  eti mema aliyoyaanza.. when? lol
   
 5. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nitaisifia Serikali yoyote ile ambayo itahakikisha wananchi wake hawafi kwa kukosa tiba stahili. Hivi sasa wananchi wa vijijini na wa kipato cha chini walio mijini wanakufa kwa kukosa fedha za matibabu. Wananchi wengi wamerudi kwenye kutumia miti shamba na hata wale wenye uwezo kiasi wameanza kutumia zaidi dawa za asili ama zile zinazotokana zinazotangazwa na akina Dr. Ndodi kwenye radio na televisheni zinazohusu kula vyakula vinavyoaminika kwamba vinaleta tiba.
   
 6. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hao ndo viongozi wa TZ, si ajabu. Wanauwezo wa kupanga matokeo.:biggrin1:
   
Loading...