jerrytz
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 5,975
- 4,264
Maafisa wawili wa serikali ya tanzania inaarifiwa kuwa walifika Malawi wiki iliyopita ili kupewa taarifa juu ya Watanzania wanane wanaoshikiriwa na serikali ya Malawi.
Watanzania hao walikamatwa katika mgodi wa madini ya Uranium wa Kayekera eneo la Karonga.
Afisa katika mpaka wa Songwe ndugu Yusufu Shaibu alisema kuwa maafisa hao wa Tanzania ambao ni Daniel Magwaza na John Njirakiza walifanya mahojiano na wana usalama wa serikali ya Malawi kutoka Karonga mpakani hapo.
" Walitaka kufahamu juu ya watu waliokamatwa na makosa yao kutokana na taarifa kwamba watu hao walikuwa wakifanya upelelezi katika eneo la Kayelekera na kwamba inadaiwa walitaka kujua kama Malawi inataka kufanya masuala ya Kinyuklia.." alisema Shaibu.
Watanzania hao wanane bado wapo katika gereza la Mzuzu nchini Malawi na watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka.
Taarifa zinasema kuwa Watanzania hao nane walikutwa na kamera.
Source: The Guardian 05 January 2017