Malawi is broke: Sends government workers on forced leave

Lenders/Development partners have withheld their money until the "cashgate" theft is dealt with acceptably, and an appropriate mechanism is put in place to curb looting in future.

What is this Cashgate theft?
 
MDF Wako kazini ila hali ni mbaya.Vikosi havina hela za kununulia mafuta kuweka kwenye magari yao.Na hawana hela za bajeti za kuendeshea shughuli zao za kila siku kama kununua vipuri n.k

Wazabuni hawajalipwa wengine wamesusa kuendelea kuhudumu zabuni za jeshi.Ni chaos.

Nadhani kuwapa forced leave anaogopa!
Cameroon na Malkia wana taarifa?
 
Hiyo hela ya kumpatia itatoka wapi?

attachment.php
 
MDF Wako kazini ila hali ni mbaya.Vikosi havina hela za kununulia mafuta kuweka kwenye magari yao.Na hawana hela za bajeti za kuendeshea shughuli zao za kila siku kama kununua vipuri n.k

Wazabuni hawajalipwa wengine wamesusa kuendelea kuhudumu zabuni za jeshi.Ni chaos.

Nadhani kuwapa forced leave anaogopa!

data umetoa wapi mkuu..
 
Kwa askari wa malawi.Ukiwapa bia tu wanatapika kila kitu hela za kulewa hawana.Ukikutana nao hata wewe watandike bia usikie wanavyobwabwaja.Hawasazi kitu.

umenitisha sana..nataka kujua ni kwanini inakuwa hivyo ua uchumi wa nchi nyingi za kiafrika unashikiriwa na kundi la watu fulani(mafisadi papa na nyangumi)..Maana kuna tetesi pia hata hapa bongo hazina imefilisiwa na serikali inategemea makusanyo ya TRA ndomana wanakuwa strictly katika kukusanya kodi
 
Tananzania nayo inaelekea huko huko uongozi mbovu sana viongozi wanachumia matumbo yao na familia zao tuu., wakirithishana madaraka kwa ukoo.,
 
mwingine wamemkomalia atoke madarakani huko thailand. uraisi raha wakati wa kampeni tu ukishaingia utakiona. si aliuza ndege ile hela aliyopata ameshamaliza?
Mzungu bwana ni noma sana, ukifanya masihara anakufix mpaka utajuta kuzaliwa
 
Cameroon na Malkia wana taarifa?

Si tu wana taarifa ila ndio kawaliza kwa kukwapua hela zao walizotoa.Walipozuia misaada kwa hasira na kutuma mwandishi wa gazeti la Daily Telegraph la uingereza kumhoji alichojibu kijeuri Joyce Banda hiki hapa nakupa kwa kizungu.

" If you want to give me something and then withdraw it, fine, I must respect your decision. I am not going to cry over it, no," she told the UK Telegraph last week.

"The donors have not walked away for the first time. They come and go and come and go but we are here, we did not die," she was quoted as saying"

 
Inabidi ikumbukwe huyu mama kaupata uraisi kibahati (kufa kufaana, hakuchaguliwa kuwa raisi) na hata ndani ya serikali na chama cha Bingu wa Mutharika hakuwa mmoja wa watu walio kuwa wakitegemea kushindania uraisi. Kwa maana hiyo ilibidi atafute njia ya kuconsolidate power na ndio muda ule ule akaaza choko choko na Tanzania.

Kwenye political science kuna nadharia inaitwa "rallying around the flag" theory kwa maana kwamba nchi ikiwa katika uhasama na nchi nyingine basi wananchi wata ungana na kumsupport kiongozi wao dhidi ya hiyo nchi zingine. Hii inasaidia kusahaulisha watu matatizo yao ya ndani. Hii iifanya kazi kwa muda kwa maana wananchi wa Malawi waliungana katika kuisema na kuiponda Tanzania.

Tatizo likaja kwamba Joyce Banda new she was making empty threats. Malawi ika lazimika kukaa mezani na Tanzania na leo Wamalawi wa kawaida wamesha sahau mgogoro wa ziwa wamekumbuka njaa zao.

Ukija kwenye swala la kuuza ndege. Pale Joyce Banda alipo uza ndege ya raisi kwa $ 15M tu watu walisha anza kuona kuna matatizo na hali mbaya sana ya kiuchumi. Kwa maana hata kwenye maisha ya kawaida ukimuona mtu anauza gari lake na kuanza kupanda dala dala ujue hali ya uchumi si mzuri. Yeye aka danganya wananchi wake kwamba amefanya hivyo kuokoa gharama.

Mama nchi isha mshinda. Ila alitegemea nini wakati alikua hana hata support toka kwa chama chake mwenyewe? Amalizie tu miezi yake iliyo baki akapumzike.
 
Oya masela nitoleeni mahali nimwoe huyo Joyce Banda ili mahali hiyo iwasaidie watu wake wasije kufa njaa!
Vp watz wenzangu nichangieni mahali nikaoe hako kaprezida kamalawi!
 
Back
Top Bottom