Malalamiko ya Watu dhidi ya Magufuri Kuhusu Zanzibar Tafsiri yake ni Nini?

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,174
1,937
Habari wana jf
kumekuwa na sintofahamu dhidi ya Rais Magufuri kukaa kimya kuhusu mkwamo wa kisiasa Zanzibar, mengi yameandikwa na baada ya kutoa msimamo wake bado mijadala inaendelea. Wapo wanaounga mkono, wengine wanapinga. Mimi nimepata maswali mengi yasiyokuwa na majibu, huenda nikapata kueleweshwa humu.
1: Hivi Rais Magufuri anaombwa aingilie mkwamo huo ili atoe amri matokeo yatangazwe, au aingie kama msuluhishi? Kama ni msuluhishi tu mbona imekuwa ni kama analazimishwa kusuluhisha mgogoro ambao yeye amekwishauona hawezi kuhusuluhisha tofauti na kurudia kura?
2: Je, huu mkwamo wa Z'bar wanasiasa wanataka kuutumia ili kuwaaminisha wananchi kuwa Magufuli hawezi chochote?
3: Je, kwanini wasioridhika na uchaguzi kurudiwa hawajaenda mahakamani kama kuna tafsiri isiyoridhisha ya kikatiba ili mahakama itoe tafsiri?
4: Hivi kweli Magufuli anaweza kuamuru matokeo ya uchaguzi Z'bar yatangazwe kwa mujibu wa Katiba ya Z'bar?
5: Endapo vyama vyote vikikubali kurudia uchaguzi wakikubaliana huo uchaguzi usisimamiwe na wale ambao tayari upande mmoja hauna imani nao peke yao bali ujumuishe watu kutoka jumuiya nyingine za kimataifa bado matokeo yatakuwa batili?
6: Sababu zilizomfanya Jecha afute uchaguzi zina ushahidi kweli?
7: Jecha alikuwa na mamlaka ya kufuta uchaguzi kikatiba?
Kweli siasa za Afrika ni changamoto. Lakini Rai yangu kwa Wazanzibari iwekeni Zanzibar mbele kwanza maslahi ya kisiasa baadae. Tazameni Iraq, Syria, Somalia leo watu wanahangaika kwa ajili ya Matakwa ya watu. Amani haina mbadala na dhambi ya vita huwa haifutiki mapema, bora tubaki na amani yetu!
 
Tutahakikisha suala la znz tunalishughulikia ili nchi iende mbele...
 
kulinda muungano kwa gharama yote ile CCM imepotoka na inauoga wa kutisha CUF ikichukua madaraka ndio mwisho wa muungano siyo kweli nadhani ndio mwisho wa dhulma vidi ya Wanzibari- bahati mubaya JPM anaugua phobia ya CUF kuvunja muungano.
 
Back
Top Bottom