Mimi nadhani hapa ni kuwa na discipline itasaidia, wazo langu kama unajijua unatumia sana internet basi tafuta mtandao unaona unafaa kwa wakati huo, weka bajeti ya mwezi kulingana na gharama kwa wakati huo, tafuta wireless modem ili iwe rahisi kutumia kwenye device yoyote nikimaanisha ukiwa na shida na internet kwenye simu basi unaunga wireless hivyo hivyo kwenye laptop, kama ofisini kwako kuna internet basi hakikisha mahitaji yako ya internet unayamalizia ofisini haswa haswa muda wa lunch au jioni kabisa after office hours hiyo itakuondolea gharama za internet, kwenye kuongea mimi nashauri tujijengee tabia ya kupiga simu pale palipo na ulazima kama kuulizia mambo fulani au kwa simu za kibiashara ambazo zitaingia faida, wengi wetu tunapiga simu halafu tunaanza story au umbea au tunaitafuta point kwa mazungumzo marefu jambo ambalo sio sahihi, mfano mimi nikipiga simu basi kuna huo ulazima na nikipigiwa simu huwa nauliza vp mbona umenipigia na kama huna point nitakuambia samahani nitumie message. Hii imenisaidia kupunguza gharama, na mtandao ninaotumia kama hujajipanga basi huwezi nipigia simu ovyo.