mpayuko senior
Member
- Sep 11, 2014
- 22
- 0
Hawa tigo ni wazi sana nimeamua kuivunja laini yao. Nimeweka vocha nikajiunga kifurushi, nimepiga simu mpaka muda umeisha ghafla inaingia meseji wamenikopesha 1300 nitalipa 1500. Sikuhitaji kukopa wala kukopeshwa. ....
Wamepunguza kifurushi cha internet cha mwezi toka 35GB hadi 5GB kwa bei ileile ya sh elfu 20. Wamenikers sana.
Wamepunguza kifurushi cha internet cha mwezi toka 35GB hadi 5GB kwa bei ileile ya sh elfu 20. Wamenikers sana.
mmh! Hizi comedy sasa. Mbona badiliko kubwa sana! Au ilikuwa promo! Ngoja nisubiri airtel sasa, maana voda kimeshanuka, laini nimeweka kwenye kikombe.
Inabidi tuweke mgomo wa kutumia hizi huduma za simu za mkononi walau wiki moja tu kila mmiliki wa simu hakuna kuweka vocha, tuwaone kama ofisini watawasha vi yoyozi, Voda wanachinja,tigo wananyonga, airtel wanaziba pumzi. loh.