Mleta mada ushauri hebu tembelea ofisi za TRA hapo huwa kuna ofisi ya Huduma na Elimu waulize maana kwa sasa utapeli umekuwa mkubwa.navyofahamu mimi ofisa wa serikali anapokuwa kikazi ni wajibu kujitambulisha na kitambulisho chake,pili TRA navyojua huwa wanatoa Waraka wa kodi kwa muhusika ili akalipie benki,tatu kodi huwa inatozwa na mzunguko wa biashara hivo ,inawezekana hao ni matapeli maana sasa hivi wamekuwa wengi.ukiona mtu anadai ni TRA hebu muombe kitambulisho ujiridhishe maana mjini matapeli ni wengi wanatafuta fursa.