Malaika na wachungaji wa mifugo usiku wa manane

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,233
16,202
Yosefu nae alifanya safari kwenda bthlehemu mkoani yudea kutokea nazareti mkoani galilaya kwa ajili ya kuhesabiwa
Pamoja na mchumba wake maria ambae alikua mjamzito.
Wlipofika huko siku ya maria kujifungua iliwadia akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume akamvika nguo za kitoto akamlaza horini mwa kulishia mifugo kwa kua hawakupata nafas katika nyumba za wageni luka 2)4-7)
Katika sehemu hizo walikuepo wachungaji wakikesha usiku mbugani kulinda mufugo yao
Malaika wa mungu akawatokea gafla na utukufu wa mungu ukawaangazia pande zote
Wakaogopa sana lakini malaika wa mungu akawaambia msiogope!! Nimewaleteeni habari njema ya furaha kubwa itakayowapata watu wote!!) Kwa maana leo hii katika mji wa daudi amezaliwa mwokozi(yesu)kwa ajili yenu ndie kristo bwana.) Na hiki kitakua kitambulisho kwenu
Mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto
Amelazwa horini

Mara kundi kubwa la malaika likajiunga na huyo malaika
Wakamsifu mungu wakisema
Utukufu kwa mungu juu mbinguni
Na amani duniani kwa watu anaowafadhili
Baada ya hao malaika kuondoka na kurudi mbinguni
Wale wachungaji wakaambiana
Twendeni moja kwa moja mpaka Bethlehem tukalione tukio hili ambalo mungu ametujulisha

Basi wakaenda mbio wakamkuta maria na yosefu na yule mtoto amelazwa horini
Walipomwona mtoto wakamwambia maria mambo yote waliyoyasikia juu ya mtoto Huyo
Wote walioisikia habari hiyo walishangaa hayo waliyoambiwa na wachungaji
Lakini maria aliyaweka hayo moyoni na kuyatafakari yote aliyoyasikia!
Wale wachungaji walirudi makwao wakimtukuza mungu
Na kumsifu mungu kwa yote waliyosikia na kuyaona kwa kua yalikua kama walivyoambiwa na malaika luka2)8-20

Hatuna budi kufurahi na kusheherekea na kumtukuza na kumsifu mungu kama wale malaika na wale wachungaji bila kujali tarehe au mwezi ambao bible haijaweka wazi wala wale malaika au wale wachungaji

Siku nane baadae alitahiriwa na kupewa jina la yesu yaani)mkombozi) ambalo alikua amepewa na malaika kabla hajachukuliwa mimba luka2)21 mathayo1)20-25)

Nawatakia nyote heri ya christmass na mwaka mpya
 
Asante sana, na kwako pia Mkuu.

Krismas ina shida
Kwa nini Biblia haitaji tarehe ya kuzaliwa kwa Yesu lakini inataja tarehe ya kufa kwake?
Kwa nini Yesu aliamuru wanafunzi wakumbuke kufa kwake na sio kuzaliwa kwake?
Kwa nini majira yanayoelezwa na Biblia siku aliyozaliwa kwa Yesu haiwezekani kuwa ni mwezi Desemba?
Kwa nini Krismas hasa ni siku ya Maovu ?
 
Ndugu kwetu tarehe na mwezi si kitu kabisa kwa kua tunamwabudu mungu katika roho na kweli
Na bible haijataja tarehe ya kufa na kufufuka kwa yesu bali imetajwa siku ya ijumaa jumamosi na siku ya kwaza ya juma baas
Pia ndugu iwe ilikua baridi au joto kwetu sio muhimu
Muhimu kwetu tunakumbuka mkombozi aliposhuka duniani kwa njia ya kipekee
 
hebu nitajie tarehe ya kufa kwa YESU
 
hebu nitajie tarehe ya kufa kwa YESU

Yesu alikufa siku ya Pasaka ya kiyajudi ambayo bado inasherehekewa mpaka Leo na wayahudi.Pasaka ilifanywa Mwezi wa NISANI TAREHE 14 KILA MWAKA.Kulingana na kalenda ya Biblia(ya Wayahudi) NISANI ni Mwezi unaolingana ,na miezi ya Machi/Aprili kwenye kalenda tunayotumia(Ya Augusto kaisari)
 
Ndugu kwetu tarehe na mwezi si kitu kabisa kwa kua tunamwabudu mungu katika roho na kweli
Na bible haijataja tarehe ya kufa na kufufuka kwa yesu bali imetajwa siku ya ijumaa jumamosi na siku ya kwaza ya juma baas
Pia ndugu iwe ilikua baridi au joto kwetu sio muhimu
Muhimu kwetu tunakumbuka mkombozi aliposhuka duniani kwa njia ya kipekee

Waefeso 5:10 unasema "Endeleeni kuhakikisha like linalokubalika kwa Bwana"
Je umehakikisha kwamba Bwana anakubali CHANZO,CHIMBUKO,DESTURI,MAZOEA ya Krismas?
 
Yesu alikufa siku ya Pasaka ya kiyajudi ambayo bado inasherehekewa mpaka Leo na wayahudi.Pasaka ilifanywa Mwezi wa NISANI TAREHE 14 KILA MWAKA.Kulingana na kalenda ya Biblia(ya Wayahudi) NISANI ni Mwezi unaolingana ,na miezi ya Machi/Aprili kwenye kalenda tunayotumia(Ya Augusto kaisari)

Bora ungekaa kimya kuliko kujitia unajua badala yake umekua kichekesho
 
Yesu alikufa siku ya Pasaka ya kiyajudi ambayo bado inasherehekewa mpaka Leo na wayahudi.Pasaka ilifanywa Mwezi wa NISANI TAREHE 14 KILA MWAKA.Kulingana na kalenda ya Biblia(ya Wayahudi) NISANI ni Mwezi unaolingana ,na miezi ya Machi/Aprili kwenye kalenda tunayotumia(Ya Augusto kaisari)

ha ha ha ha ha NISANI PATROL au? ok nisikukatshe tamaa nipe andiko nisome linalosema YESU alizaliwa mwez wa 3/4 tarehe 14
 
Tatizo lao hawajui tunasherekea nini wao hufikiri tunasherekea tarehe na mwezi
 
Back
Top Bottom