Makusanyo ya kodi yanavyoimarika chini ya rais Samia

Sep 17, 2021
39
84
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema usimamizi mzuri wa sera za kiuchumi na fedha sambamba na kujenga mahusiano mazuri kati ya walipa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kumechangia kuimarika kwa makusanyo ya kodi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 13, 2022) wakati akisoma hotuba ya kuhitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake pamoja na Mfuko wa Bunge, jijini Dodoma. Bunge limepitisha kwa kauli moja bajeti hiyo.

“Kwa mfano, Desemba 2021, TRA ilikusanya shilingi trilioni 2.51 sawa na ufanisi wa asilimia 109 wa lengo la kukusanya shilingi trilioni 2.29 katika kipindi hicho. Kuvunjwa kwa rekodi hiyo ya makusanyo ya kodi ni kielelezo tosha cha kazi nzuri anayoifanya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.”

Waziri Mkuu amesema kuwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) zinaonesha kuwa katika kipindi cha Machi, 2021 hadi Februari, 2022, Serikali imeweza kuvutia na kusajili jumla ya miradi ya uwekezaji 294. “Miradi hiyo inatarajiwa kuwekeza mtaji wa thamani ya dola za Marekani bilioni 8.13 na kutoa ajira kwa watu wasiopungua 62,000.”

Amesema kuwa Afrika inamtazama Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa miongoni mwa viongozi waliochangia kuliweka bara hili katika ramani nzuri ya dunia kutokana na namna alivyofanikiwa kushughulikia suala la UVIKO-19.

Ameongeza kuwa mkopo nafuu wa sh. trilioni 1.3 kutoka IMF umeiwezesha Serikali kupeleka sh. bilioni 100.58 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za sekondari 214. “Taratibu za kuanza ujenzi huo, zinaendelea kwenye kata za majimbo yote nchini.”
FEAB1BE9-71B8-40B8-B62D-8DA175459295.jpg

“Tumepeleka shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari mpya za wasichana kwenye mikoa 10 ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kujenga shule moja ya sekondari ya wasichana kwa kila mkoa wa Tanzania Bara.”
 
Sidhani kama kodi inakusanywa ipasavyo.

Hakuna mtu anafurahia kuilipa.

Ni kudanganyana tu kwamba mtoza ushuru anaweza kuwa rafiki wa mlipa kodi na mambo yakaenda. Hiyo haipo.
 
🐒🐒🐒
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema usimamizi mzuri wa sera za kiuchumi na fedha sambamba na kujenga mahusiano mazuri kati ya walipa kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kumechangia kuimarika kwa makusanyo ya kodi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 13, 2022) wakati akisoma hotuba ya kuhitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake pamoja na Mfuko wa Bunge, jijini Dodoma. Bunge limepitisha kwa kauli moja bajeti hiyo.

“Kwa mfano, Desemba 2021, TRA ilikusanya shilingi trilioni 2.51 sawa na ufanisi wa asilimia 109 wa lengo la kukusanya shilingi trilioni 2.29 katika kipindi hicho. Kuvunjwa kwa rekodi hiyo ya makusanyo ya kodi ni kielelezo tosha cha kazi nzuri anayoifanya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.”

Waziri Mkuu amesema kuwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) zinaonesha kuwa katika kipindi cha Machi, 2021 hadi Februari, 2022, Serikali imeweza kuvutia na kusajili jumla ya miradi ya uwekezaji 294. “Miradi hiyo inatarajiwa kuwekeza mtaji wa thamani ya dola za Marekani bilioni 8.13 na kutoa ajira kwa watu wasiopungua 62,000.”

Amesema kuwa Afrika inamtazama Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa miongoni mwa viongozi waliochangia kuliweka bara hili katika ramani nzuri ya dunia kutokana na namna alivyofanikiwa kushughulikia suala la UVIKO-19.

Ameongeza kuwa mkopo nafuu wa sh. trilioni 1.3 kutoka IMF umeiwezesha Serikali kupeleka sh. bilioni 100.58 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za sekondari 214. “Taratibu za kuanza ujenzi huo, zinaendelea kwenye kata za majimbo yote nchini.”View attachment 2186305

“Tumepeleka shilingi bilioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari mpya za wasichana kwenye mikoa 10 ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kujenga shule moja ya sekondari ya wasichana kwa kila mkoa wa Tanzania Bara.”
Huu ni uongo, ujenzi wa shule mpya wasichana kila mkoa ni Mkopo wa Benki ya dunia kupitia mradi uitwao SEQUIP.
Hapo hakuna makusanyo ya kodi katika ujenzi wa hizo shule
 
Hongera sana PM makini kuwahi kutokea Tz
 
Back
Top Bottom