Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,411
Serikali yaombwa kusaidia kuzuia Makundi ya wanyamapori yanayoingia kwenye makazi ya watu na kutishia uhai.
Wakazi wa vijiji vya Kata ya Tingatinga na vingine katika Wilaya ya Longido wameiomba serikali iwasaidie kuzuiya makundi ya wanyamapori wakiwemo Tembo, Simba na Chui wanaodai wa kufunguliwa kutoka kwenye moja ya hifadhi ambao wanaingia katika makazi ya watu na kufanya uharibifu mkubwa kwenye mashamba,mifugo na kutishia uhai wa bindamu.
Wakizungumza na ITV wakazi wa Wilaya ya Longido wamesema wanyapori wamekuwa tishio kwenye mashamba, mazizi ya mifugo na makazi ya binadamu kwani wameharibu mazao kula mifugo na inadaiwa kuwa wanyama hao wanafunguliwa kutoka kwenye moja ya hifadhi lakini kila wanapo toa taarifa hazifanyiwi kazi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, SABORE ole MUREIMET amesema wanyamapori wamehamishwa kutoka wilaya ya jirani na wao kama viongozi wa Wilaya ya Longido hawakushirikishwa na mpango huo lakini wanaendelea kuwasiliana na uongozi wa serikali ili kupata ufumbuzi.