Makundi ya wanawake katika Mahusiano.

Makundi ya wanawake katika Mahusiano.

Tetra

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
1,526
Reaction score
771
Si kila mwanamke yuko sawa na mwanamke mwingine,,wanatofautiana kama ambavyo wanaume wanavyotofautiana.Kuna baadhi ni

1:: WAGUMU
wanakumbuka kila kitu mlichofanya nae si leo tu bali milele!
Yuko tayari kuacha uhusiano mwanaume akiamua au hali ikimlazimu mf.mimba kwa mtu ambaye hakumtarajia,kulazimishwa kuolewa na mwingine,kusalitiwa na mwanaume,kudanganywa n.k lakini ni wagumu wa kusahau mliotenda nae na atakukumbuka Daima.

2:: WEPESI
wanasahau kila kitu ulichofanya nae mara tu unapomwambia leo tumeachana.Ni kana kwamba ulichelewa kuondoka.
Usidhani ataumia ukimuacha,tena atashukuru Mungu amemsaidia.

3:: WAKUTAZAMA
baadhi wanafaa kutazamwa tu huko huko waliko ila usiombe kuishi nao utajuta.Hawa ni wa kutazama tu.Ukiwaona wanavyopendeza,maneno matamu kinywani lakini ni wa kutazamwa tu.

4:: SIO BEI CHEE
wanajiheshimu sana sio wa kuparamia tu kwa sababu we ni handsome au una pesa unadhani atababaika La! Anajitambua thamani yake.Amefundwa akafundika,yuko makini na maisha yake,,ukimfuata kwa papara ya ngono utaishia kupewa ushauri

5:: BEI NAFUU
hawa wapo wakati wowote,hawasumbui ukiwahitaji wanapatikana tu.Ni wa starehe.Ni wa "acha longolongo sema una shilingi ngapi"

6:: WAANGAVU
ni wajuzi wa kubadili maisha ya mwanaume kifikra na kimaisha.Wanajua kumtunza mwanaume kwa mbinu nyingi akasawazika kiakili,akasahau taabu alizopitia,akang'aa na kufanya uhusiano utokwe chozi la furaha.Humfanya mwanaume aone ameishi miaka yote!!

7:: VING'ANG'ANIZI
ingawa kundi hili ni dogo sana ukilinganisha na wanaume (wanawake ni shahidi ktk hili) wanawake wa aina hii wakikung'ang'ania utajuta kuzaliwa.Ni wasumbufu,hawakubali kukuacha hata utamke maneno mabaya kiasi gani.Hata utoe talaka ni kazi bure atakufuatilia tu ni yeye tu anajua kwa nini anakung'ang'ania
=
 
Kuna aina hii hapa:
8. Ving'amuzi
Hawa wapo kidijitali zaidi, wao wanakamata channel pindi tu utakapolipia. Kimsingi pesa kwanza, huduma baadae tena utaipata bila chenga.
 
Kuna aina hii hapa:
8. Ving'amuzi
Hawa wapo kidijitali zaidi, wao wanakamata channel pindi tu utakapolipia. Kimsingi pesa kwanza, huduma baadae tena utaipata bila chenga.

watu8
hahaa nimeipenda hii
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom