Makundi matatu ya vijana wa Tanzania

Makundi matatu ya vijana wa Tanzania

ZOPPA

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2017
Posts
2,752
Reaction score
2,928
*1.WANAOISHI JANA*
Kuna hili kundi la kwanza la vijana ambao wao wanaishi jana,maisha yao yote wamewekea umakini kwenye mambo yaliyowatokea jana, nilifeli shule, niliachwa,nilianzisha Biashara ikafa, nilipata Ajali, nilidhurumiwa.Matukio haya yote yalitokea jana. Kundi hili huwa Ni kazi sana kufanikiwa mpaka watakapoamua kusema imetosha, yajana yamepita sasa naanza upya hapo maisha yao yataanza kubadilika.Na hii nikwasababu kundi hili wengi huwa wamekata tamaa wengine matumaini yao yamebakia kwenye BETTING

*2.WANAISHI KESHO*
Kundi hili pia ni kundi la vijana ambao wanaishi kesho,unakuta kijana kila kitu akiambiwa fanya anasema nitafanya kesho, anzisha biashara kesho, akionyeshwa fursa atakwambia bado najipanga nitafanya kesho, vijana hawa sasa kwenye swala la mafanikio sio tu kutokufanikiwa bali huwa wanakufa na ndoto zao Maishani. Lakini katika kundi hili pia wapo vijana ambao akifanikiwa kidogo tu anaanza kufanya matanuzi unakuta kijana hata hajafikia kumiliki simu ya iPhone sijui nini plus ya mamilion lakini anataka kumiliki leo wakati hata Biashara hana, mdada unamkuta hana mbele wala nyuma Lakini kichwani anaweaving la laki tatu khaa acha kuishi kesho yako wakati bado

*3.WANAOISHI LEO*
Hili ni kundi la mwisho la vijana ambao huwa wanafanikiwa sana maishani, hawa huwa wanaishi leo nikiwa na maana akipata fursa ya biashara anaanza leo hata kama ataanza kidogo, haangalii yaliotokea jana, haangalii alishindwaje jana anaangalia leo, hawa kama leo yuko kwenye maisha ya kuvaa nguo za kawaida atavaa tu bila kuangalia nani atamuonaje wala atamfikiriaje.Hawa huwa washindi.Hawa huwa liwezekanalo leo wanalifanya leo hawangoji kesho

*KIJANA KESHO YAKO INAANDALIWA LEO*
 
aiseeh mimi ni mzee kesho, alafu ikifika kesho naanza kusikitika kwa nini sikufanya jana.
 
Unapoiwaza kesho , jana yake ndiyo leo.

Message sent and received
 
Aliyepiga deal la trilion 1.5 naye yupo kundi gani?

Moyoni unajua. Ila ndo nyie Kama hujatumwa basi bangi. Nahisi unamatumaini mbowe akiwa Rais Atagawa Hela. Ukweli Mchungu ni kuwa TZ. Rais mzalendo atabaki JPM. Ndo Mana mnakoroma sana. Mnaona Ndege. Na zingine Zaja. Wala kimya. Sasa wewe tuonyeshe. RUZUKU na ofisi. Uwiiiiiii mayoooo. Aikambe.
 
Ha ha ha ha
Ww ndiyo msukule original unayelishwa unga wa ndere. Nafikiri ulipata mgao wa trilion 1.5 alizokwapua papa fisadi. Mtu kafuta ajira (walimu wa arts, afya na NIDA), Kafuta fao la kujitoa, Kaongeza kimabavu toka 8%-15% bodi ya mkopo ili ale na wapambe, hakuna nyongeza ya mshahara wala kupandishwa madaraja, sasa hiv kaona watu wanamjudge kapitisha sheria ya kulipa zaid ya milion 2 kwa wenye blog, website, youtube na forum (Hata ww msukule unayeshabikia huku unatumia JF huenda JF ikafa kwa sheria za kijinga), Kaiba mpaka hela za rambi rambi. Pole sana. Unajivunia ndege wakat ni mbovu na zinaendeshwa kwa hasara. Ww mwenyew sidhani km umepanda ndege.
 
Good
 
Back
Top Bottom