Acceptable
Senior Member
- Oct 7, 2020
- 153
- 302
Mama ameingia na upepo mzuri sana kwa kutoa matumaini kwa Watanzania kupitia maneno tu watu wamefurahi na kusubiri vitendo sasa.
Inaonekana kuna kundi kubwa sana la watu walikuwa na majonzi na simanzi katika nchi yao kwa muda mrefu sana. Kama tunavyojua au kuaminishwa kwamba maneno huumba lakini yanaweza kuumba kitu kizuri au kibaya.
Ninachokiona hapa watu wanamsifu sana mama ila napenda kutoa angalizo kwa wasaidizi wa mama wamwambie; Mama asipokuwa makini nae watamchukia kama walivyokuwa wanamchukia Anko. Sababu zitakazofanya watu wa mchukie ni zilezile zilizofanya watu wamchukie Anko. Lakini kuna makundi makuu mawili haya yanashauku kubwa sana ya kupata unafuu wa maisha nayo ni:
Kundi la vijana waliomaliza vyuo wana matumaini kwamba wataajiriwa na mama baada ya kula msoto wa kukaa nyumbani kwa zaidi ya miaka 4. Huku wenye connection na bahati za mitende wakipata nafasi za kazi kwa kudonoa donoa.
Kama ikitokea Mama asiwaajiri vijana waliohitimu vyuo mbalimbali lazima watamgeuzia kibao kama walivyofanya kwa Anko, watamchukia kwasababu hakutakuwa na tofauti yoyote kati yao.
Kundi la wafanyakazi ambao kwa miaka mitano hawajapata nyongeza ya mishahara. Natumaini yao kwasasa yapo kwa Mama kwamba atawaongezea mishahara yao. Kama itatokea Mama akashindwa na yeye kuwaongezea mishahara basi na yeye watamchukia kama walivyokuwa wanamchukia Anko.
Muda utaamua kwamba nafuu na afadhali ipi ni bora kuliko nyingine.