Makumbusho ya Taifa yanapokosa kumbukumbu muhimu!

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Sasa kumekuwepo na sintofahamu ya nani mchoraji hasa wa nembo ya taifa hili kubwa; na lenye historia iliyotukuka.
Hii ni baada ya kuibuliwa kwa mgonjwa aitwae mzee Ngosha ambaye sasa amelezwa katika hospitari ya Muhimbili.

Kwanza kabisa nimshuru sana mzee Ngosha bila kujari kama ndiye mchoraji hasa au sio, maana kama yeye asingedai hivyo huenda isingefika mahari kama taifa tukamfahamu mtu aliyechora kitu kikubwa, na chenye heshima kwa taifa hili.

Naleta mada hii ikiwa ni muda mfupi tu tangu ya itokea familia nyingine ya mzee Jeremiah Kabati ambayo kwa kweli ina maelezo mengi zaidi, ambayo ukiyasikiliza kwa makini hakika yanasadikisha kuwa huenda ndugu yao ndiye mchoraji halisi wa nembo yetu ya taifa.

Yote ni yote ilimradi mpaka sasa tuna watu wawili ambao wote wanadai ni wachoraji wa nembo ya taifa ilihali watu hao sio kwamba walishirikiana kuchora hicho kitu! Huu ni mgogoro Mkubwa!

No rahisi mno kwa watu wemye mawazo mepesi kukimbilia kudhani kuwa huu mgogoro ni wa watu hawa wawili tu na familia zao!
Lakini ukweli ni kwamba huu ni mgogoro wa watanzania wote ambao kimsingi ndio wenye kutaka kujua historia yao.

Nikiachana na familia hizo mbili au hata zaidi akitokea mwingine; hebu sasa nirudi kwa wenzetu hawa wa makumbusho ya taifa.
Mimi nadhani hapa ndipo kilipo kiini cha tatizo lenyewe!
Kwa hali ilivyo sasa,; na inavyoendelea kuwa, huenda hawa jamaa hawana picha za mtu aliyechora nembo ya taifa.

Ninavyofahamu mimi ni kwamba; wasanii wengi walishiriki katika kuchora, na kupeleka michoro yao ya ubunifu kwa serikali hata hivyo ni mchoro mmoja tu ambao ulishinda.
Sasa basi watanzania tulitegemea pale makumbusho ya taifa kuziona picha za wasanii wote walioshiri zoezi la kuipata nembo ya taifa.
Tena kila mmoja na mchoro wake, pamoja na mchoro ulioshinda michoro yote na picha ya mchoraji wake.

Sasa kama haya ninayosema hayapo hivyo; nini maana ya kuwa na makumbusho ya taifa?
Makumbusho gani hii inayokosa kumbukumbu muhimu kama hizo?
 
Kwanza kabisa nimshuru sana mzee Ngosha bila kujari kama ndiye mchoraji hasa au sio, maana kama yeye asingedai hivyo huenda isingefika mahari kama taifa tukamfahamu mtu aliyechora kitu kikubwa, na chenye heshima kwa taifa hili.
 
Sasa kama haya ninayosema hayapo hivyo; nini maana ya kuwa na makumbusho ya taifa?
Makumbusho gani hii inayokosa kumbukumbu muhimu kama hizo?


Mtunzi wa wimbo wa taifa na designer wa bendera ya pia watafutwe wajulikane

Ikiwezekana na wale watunzi wa
  • Tazama ramani utaona nchi nzuri, yenye...
  • Tanzania Tanzania nakupenda kwa...
Kama haitakuwa kikwazo vilevile :D
  • Chama chetu cha mapinduzi chajenga nchi...
  • Chama cha mapinduzi Tanzania eeeh!!
  • Ohh TANU yajenga nchi, Ohh Tanu yajenga nchi
 
Uko vizuri..Hiyo makumbusho ya Taifa inabidi wawe serious aisee katika kutunza kumbukumbu muhimu za nchi hii
 
Angalizo zuri hilo

Makumbusho ya Taifa ina kazi zifuatazo

"It is a scientific educational and cultural institution charged with the duties of collecting, conserving, displaying, and researching on all materials relating to Tanzanian’s cultural and natural heritage."

Kama watashindwa kuclear huu utata kwa taarifa sahihi basi Makumbusho ya Taifa si chombo kinachofanya mambo yake kwa kufuata misingi ya science.

Wanawajibu kujibu hili.
 
Back
Top Bottom