R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,575
Hii hapa makumbusho ya kwanza kuwa chini ya maji, sasa watembeleaji watatakiwa kuogolea kushuhudia maajabu yake
Tayari Bara la Ulaya wameweza kufanya kitu cha ajabu zaidi baada ya kuanzisha Makumbusho maalum ambayo ipo chini ya bahari. Kwa hatua hiyo watembeleaji itawataka kutembelea humo kwa njia ya kuogelea na mavazi maalum ili kushuhudia maajabu ya makumbusho hayo chini ya maji.
Kwa mujibu wa mtandao wa Kimataifa wa (CNN) umefafanua kuwa Ulaya inakuwa bara la kwanza kuwa na makumbusho hiyo ya chini ya bahari katika kisiwa cha Lanzarote.
Masanamu hayo yanavyoonekana chini ya maji.
Makumbusho hayo ni masanamu mbalimbali yaliyoingizwa humo huku yakiwa na kumbukumbu ya watu maarufu waliowahi kuwapo duniani ambapo msanii wa masanamu hayo amebainisha kuwa kuwapo baharini humo ni Ulinzi wa bahari.
Msanii wa kimataifa Jason deCaires Taylor aliyetengeneza masamu hayo amebainisha kuwa, ametengeneza masanamu hayo kwa mazingira ya kirafiki ya saruji huku akiamini kuwa, yataongeza uelewa wa masuala ya bahari.
Jason deCaires Taylor akiwa chini ya maji kwenye masanamu aliyotengeneza.
Masanamu hayo yapo chini ya umbali wa mita kati ya 12 na 15 chini ya bahari huku yakionekana kama kundi la watu (sanamu) wakitembea chini ya mawimbi.
Jason deCaires Taylor akitengeneza sanamu zake.
Muonekano wa eneo moja wapo katika kisiwa cha Lanzarote.