MAKUBWA YA MICHEZO 2017 TANZANIA

John Walter

Member
Aug 14, 2017
64
62
Walter Habari imekuletea Matukio ambayo yameacha alama katika soka.

Simba, Yanga, kubadili mfumo wa uendeshaji wa vilabu vyao
Kubadilisha uendeshaji wa klabu kutoka uanachama kwenda mfumo wa hisa Simba wameshampata mwekezaji ambaye ni mfanya biashara maafurufu Mohammed Dewji ‘Mo’ ambapo inaaminika kwamba timu itaendeshwa kisasa zaidi na kuleta mafanikio kwenye klabu hiyo ambayo yatachangia pia mafanikio ya timu ya taifa.
Yanga wameshatangaza kuanza mchakato lakini bado hawajafikia hatua ambayo watani wao wa jadi wameshaifikia, tayari kamati ya kusimamia zoezi la mchakato wa mabadiliko imeshatangazwa.
Msuva, Banda, Maguli wapata vilabu vya nje
Simon Msuva anafanya vizuri akiwa na klabu yake ya Hassan Difaa El Jadida ya Morocco, Abdi Banda pia anafanya vizuri kwenye klabu ya Baroka akiwa ameanza kwenye kikosi cha kwanza katika zaidi ya mechi 10 kati ya 15 za mzunguko wa kwanza ligi kuu y Afrika Kusini lakini kwa upande wa Maguli yeye amesaini mkataba wa kucheza Polokwane City ya Afrika Kusini.
Thomas Ulimwengu alifanikiwa kwenda Sweden lakini kwa bahati mbaya akapata majeraha makubwa yaliyomfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Zanzibar kupewa na kupokwa uanachama wa CAF (Mrch 16-July 21, 2017)
Machi 16, 2017 ilikuwa ni siku ya furaha kwa Wazanzibar ambapo katika mkutano uliofanyika Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) lilitangaza kuwa Zanzibar mwanachama mpya kamili wa 55 wa CAF.
July 21, 2017 ni siku ya huzuni kwa Wazanzibar baada ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kuwapokonya Zanzibar uanachama wa kudumu wa 55 wa CAF, ambapo Rais wa Shirikisho hilo Ahmad Ahmad alisema haiwezekani nchi moja (Tanzania) kuwa na wanachama wawili kwenye shirikisho hilo, hivyo uanachama huo umedumu kwa siku 128 tu tangu Machi 16 hadi July 21, 2017.
Mwenyekiti wa Yanga ajiuzulu (May 22, 2017)
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji aliamua kujiuzulu nafasi yake kutokana na kesi mbalimbali zilizokuwa zikimkabili (hazihusiani na masuala ya soka) pamoja na afya yake kutokuwa sawa kwa kipindi hivyo hivyo akaona hatoweza kuitumikia klabu kikamilifu. Manji aliandika barua ya kujiuzulu kwa uongozi wa klabu na hadi sasa Yanga ipo chini ya mikono ya Makamu Mwenyekiti Clement Sanga.
Victor Wanyama ndani ya Ndondo Cup (June 24, 2017)
Star huyo wa kimataifa wa Kenya anaecheza soka Tottenham alitembelea mashindano ya mchangani maarufu kwa jina Ndondo yanayondaliwa na kuratibiwa na Clouds Media Group. Wanyama alishuhudia mechi kati ya Faru Jeuri vs Kauzu FC. Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ilimpa heshima Wanyama kwa kuipa jina la Wanyama moja ya barabara za mitaa ya Ubungo lakini baadae kibao cha jina la Wanyama liliondolewa kwenye barabara hiyo kwa madai kwamba taratibu hazikufuatwa.
Rais wa TFF na Katibu Mkuu kutuhumiwa kesi za utakatishaji fedha (June 28, 2017)
Aliyekuwa Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa bado wapo ndani wakiendelea kusubiri shauri lao la makosa ya utakatishaji fedha inayowakabili pamoja na aliyekuwa mhasibu wa wakati huo.
Rais wa Simba na Makamu wake kushikiliwa na jeshi la polisi (Juni 29, 2017 walifikishwa mahakamani)
Rais wa klabu ya Simba Evance Aveva na Makamu wake Geoffrey Nyange Kaburu nao pia wanashikiliwa na jeshi la polisi wakituhumiwa kwa makosa ya kutakatishaji fedha.
Simbu aipa heshima Tanzania kwenye riadha (alirejea Tanzania August 15, 2017)
Felix Simbu alifanikiwa kurudi na medali ya shaba kutoka London kwenye mashindano ya riadha ya Dunia (IAAF World Championship 2017) baada ya kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Tamirat Tola (Ethiopia) aliyemaliza nafasi ya pili na Geoffrey Kirui (Kenya) aliyeibuka mshindi wa mashindano hayo kwa upande wa wanaume.
Kocha wa zamani wa timu ya taifa afariki Dunia (December 6, 2017)
Aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Joel Bendera wakati Tanzania ilipofanikiwa kufuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali za mataifa ya Afrika nchini Nigeria mwaka 1980, imepita miaka 37 tangu Tanzania ifuzu katika mashindano hayo lakini bado haijafanikiwa kushiriki tena fainali hizo.
Bendera pia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za kiserikali enzi za uhai wake ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na kuwa mkuu wa mkoa katika mikoa tofauti.
Zanzibar Heroes kucheza fainali CECAFA Senior Challenge Cup (December 17, 2017)
Licha ya kutofanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo, kikosi cha Zanzibar Heroes kilionesha kiwango bora katika mashindano hayo kwa kutoa ushindani wa kweli kikipoteza mechi mbili, walipoteza mchezo mmoja katika hatua ya makundi dhidi ya Morocco na mchezo wa fainali kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya kufungana 2-2 katika dakika 120.
Everton kuja Tanzania (July 12, 2017)
Tanzania iliingia katika vitabu vya historia baada ya kutembelewa na klabu ya Everton inayoshiriki ligi kuu England, Everton walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kwenye uwanja wa taifa ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya kwa Everton. Klabu hiyo ilikuwa na wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza akiwemo Wyne Rooney star wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England.
Mwanariadha Ismail Juma kufariki dunia [Decemba 1 2017]
Ajali ya fuso ilikatisha ndoto zote za mwanariadha huyu.

Ni mshumaa uliozimika ghafla,kwani ndio mwanariadha ambaye alifanikiwa kwenye ubora wa dunia.
Mwanariadha aliyekuwa anachipukia katika mbio za nusu Marathon, taarifa hiyo iliwachanganya viongozi wa riadha . Kifo cha Mwanariadha Ismail Juma kimekatisha ndoto yake ya kwenda Jumuiya ya Madola.
Kwa heri 2017 hakika sisi wanamichezo tutakukumbuka kwa mengi, karibu 2018…
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom