Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 65,127
- 111,652
Katika uvamizi wa Russia unaoendela Ukraine ni kweli sehemu kubwa ya Ukraine itageuzwa magofu na mabomu ya Russia lakini hilo halikuwa lengo la Putin, tangazo la Putin la kuanzisha vita ilikuwa ku "de-nazify" na kuwaondoa nationalists . Je ameweza kufikikia lengo hilo? kuiondoa serikali ya Ukraine mpaka sasa? Jibu ni hapana na uwezekano huo unazidi kuwa finyu kadri muda unavyosogea kwa sababu sasa majeshi ya Russia yanarudishwa nyuma kuanzia Kiev na miji mingine.
Kama utapita muda mrefu huku Putin akishindwa kumuondoa Zelenskyy na serikali yake na kuweka kibaraka wa Moscow kama ambavyo lilikuwa lengo kuu la uvamizi huu itabidi kufanya mazungumzo serious tu.
Peace deal itakuwa kati ya Putin arudishe Majimbo ya Mashariki ya Ukraine aliyoyachukua kuanzia mwaka 2014 na Ukraine ikubali isijiunge na NATO au achukue hayo majimbo matatu na aiache Ukraine iamue mambo yake itakovyojisikia. Kuna uwezekano finyu sana ataendelea kuishikilia Eastern Ukraine na pia kuizuia Ukraine isijiunge NATO.
Baada ya hii vita Russia na Ukraine kuna uwezekano mkubwa wanarudi walipokuwa kabla ya 2014 au kwenye "Square one".