Makosa ya Dr Slaa

Mtoto Wabibi

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
451
294
Katika siasa za upinzani limeonekana pengo la Dr slaa. Lakini nimeshindwa kuelewa. Kwako Dr

1: Hivi kwanini hukuwa na vijana wako (watiifu) kwako?..Je ulishindwa hata kujenga mizizi kwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA?

-hata wakuu wa shule wa vyuo, wabunge, mawaziri na wengineo wanakuwa na vijana wao wanaowapa information na kulinda nafasi zao.Hata ikitokea ishu ni rahisi kupigana nayo au kuandamana.

-Hata viongozi wa dini wana Network za vijana wao wanaolinda position zao mfano akina Gwajima, Lusekelo

-Kwa mwanasiasa mkubwa kama wewe ndio unahitaji uwe na vijana wako wengi ambao wanalinda maslahi yako kisiasa na nafasi ulionayo.Pia kwa ulinzi wako binafsi na kukupatia taarifa ( maspy binafsi) na sio kuokoteza tu hata information. wewe ulikuwa sio wa kuomba walinzi kwa gwajima wala kulalamika hovyo kusuhu ulinzi wako binafsi.hadi inafikia unaogopa kupanda jukwaani. Hebu siku itokee polisi wamkude mbowe kama walivyofanya kwa lipumba uone shughuli yake au hata maalim seifu tu.

-mbowe sio mjinga kuanzisha red briged....! na kuwatumia watu kama nyie.
-Kweli umeshindwa kuwa na nework ya viongozi wa serikali na chama ambao watakulinda na kukupigania endapo utapata msukosuko kisiasa?
- Zitto mahakama ilimlinda sana kwenye ishu yake na chadema na zile zilikuwa ni mbinu tu za Zitto.

2: Je ulishindwa kuwekeza katika sector mbali mbali nje ya siasa? Je ulishindwa hata kuwa na makampuni makubwa tanzania? au kuwa mfanyabiashara mkubwa?

-Kwa level uliyokuwepo ulijisahau na kumwamini mbowe na ajira yako. Ulishindwa kusoma tu hata kwa zitto au lowasa?

3: Je ulikuwa huwezi fitina za kisiasa? Fitina za kulinda nafasi yako au kupata zaidi ya ulichonqcho. Au lowasa alikuzidi fitina? siasa ni wanja wa fitina.
-Ulishindwa kusoma kwa zitto na mbinu zake za kutaka uenyekiti? Mbowe angezubaa tu zitto angemchomoa.hakuna mtu anayependa kushuka chini kimadaraka kama alikuwa juu. au kwa lowasa na kugombea uraisi?

Haya mambo matatu makuu ambayo yamekupoteza kisiasa. Ilikuwa vizuri endapo ungetoka chadema na team yako (yaani wanachama na viongozi). Hivyo kujenga tena msingi ni vigumu. Ulijisahau sana kwenye siasa na kuona kama ajira yako ya kudumu.Ukasahau kuna fitina sana huko.Heshima kwa J.kikwete,Lowasa, zitto,Mbowe, Maalim seifu,membe na Dr shein......! mngemfundisha na huyu siasa. Yani katibu mkuu wa zamani chadema umeniangusha na isitoshe umepotea jumla.

Nimemisi kukuona jukwaani.Karibu uanze tena hujachelewa hapo uliteleza tu.
 
Back
Top Bottom