Makosa: Sakata la kusimamisha watumishi kazi halina kichwa wala miguu! Imekuwa 'fashion'

Cheo ni dhamana. Period! Watu wamejisahau sana na kudhani kuwa vyeo hivi ni mali yao. Kama hao waliofukuzwa ni ndugu zako na mlikuwa hamjaiba sawasawa basi shauri yenu. Hamna hatimiliki na vyeo hivi.
 
Happy 10th anniversary on JF Mzee!!!
Salute!!!!!
Kwa kweli watanzania tunahitaji maombi. Zama zilizopita kelele kuwa serikali inacheka tu tulikosoa sasa serikali inajihadi kurudisha nidhamu ya kazi tunalalamika. Hivi tunajua tunachokitaka au ni fashion kukosoa
 
Inashangaza kiongozi unaamka asubuhi na kwenda kuvamia sehemu kisha kusimamisha watu kazi huku ukitoa sababu za ajabu ajabu! (Hapa sitamgusa waziri mkuu maana yeye anatenda haki na kutoa sababu za dhahiri pia Mwigulu Nchemba naye anajitahidi)

Ila hao wengine wanaosimamisha bila kuwa na evidence za kutosha huku wengine wakiishia kutoa sababu ya utendaji usioridhisha bila kutoa ushahidi wa dhahiri, wanapima madhara yake kweli?

Ummy Mwalimu alikurupuka sana kuwasimamisha kazi vigogo wa msd kwani kila hatua ya utekelezaji wa manunuzi ya vitanda ilikuwa wazi kabisa! (Nitakuja kuweka evidence hapa) Nahisi hakupata muda wa kupitia makabrasha yote na mzigo ulioagizwa!

Joyce Ndalichako naye ameenda kwenye mfumo uleule tena yeye akisema "utendaji usioridhisha" anathibitisha vipi? Ametumia vipimo gani kuwatia vigogo wa HESLB hatiani? (Nitafafanua jinsi alivyokiuka sheria kuwasimamisha kazi) Ukimsimamisha mtu kazi ni lazima uwe na ushahidi wa dhahiri kabisa! Siyo kukimbilia tu kuchukua hatua!

Rais Magufuli mathalan mkurugenzi wa MNH alimrudisha wizarani baada ya kukosa ushahidi wa moja kwa moja kumsimamisha kazi! Alishajifunza na ndo maana akitaka kumuondoa mtu kwa sasa kunakuwa na mjadala mzito kwanza na wasaidizi wake! Kosa hasa la mkurugenzi wa HESLB ni lipi? Ummy Mwalim alisimamisha watumishi akiwa kwenye kupanga vitanda MNH bila hata kuipitia taarifa ya manunuzi kinagaubaga! Au ndo kutoa pasi ya 'jipu'?


Naona sasa imekuwa fashion lakini serikali itagharamika kutokana na haya!

We ni mmoja wa taka taka na wajinga ndani ya Bavicha!
Ni wazi wewe hujui ulicho andika bali unaandika tuu bila kufanya utafiti? Hivi ulimsikiliza Dr ndalichako? Hivi ulimsikiliza Ummy?

Ngoja nianze kukujuza makosa ya mkurugenzi wa HESLB na wakurugenzi wenzie watatu!

Kwanza unatakiwa kujua kuna ukaguzi wa ndani ulifanyika kuanzia 2009-2013 madhaifu yafatayo yalibainika.

Kwanza kulikuwa na upotevu wa zaidi ya billion 3.

Pili ilibainika kuna wanafunzi wanao pata mikopo mara mbili!

Tatu imebainika kuna wanafunzi ambao walishamaliza masomo lakini wanaendelea kupata mikopo.

Nne kuna wanafunzi waliokuwa wanasoma nje kwa miaka minne lakini wanapewa mikopo zaidi ya miaka saba sasa!

Tano imebainika kuwa kuna wanafunzi ambao hawana usajili lakini wamepewa mikopo.

Sita kuna wanafunzi wasio na sifa za kupewa mikopo lakini wamepewa!

Kuhusu MSD ...
Waliosimamishwa kazi ni kutokana na upotevu wa mabillioni ya pesa hapo MSD..

Kwa hayo ulitaka wachekewe?
 
Back
Top Bottom