G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,595
- 36,017
Inashangaza kiongozi unaamka asubuhi na kwenda kuvamia sehemu kisha kusimamisha watu kazi huku ukitoa sababu za ajabu ajabu! (Hapa sitamgusa waziri mkuu maana yeye anatenda haki na kutoa sababu za dhahiri pia Mwigulu Nchemba naye anajitahidi)
Ila hao wengine wanaosimamisha bila kuwa na evidence za kutosha huku wengine wakiishia kutoa sababu ya utendaji usioridhisha bila kutoa ushahidi wa dhahiri, wanapima madhara yake kweli?
Ummy Mwalimu alikurupuka sana kuwasimamisha kazi vigogo wa msd kwani kila hatua ya utekelezaji wa manunuzi ya vitanda ilikuwa wazi kabisa! (Nitakuja kuweka evidence hapa) Nahisi hakupata muda wa kupitia makabrasha yote na mzigo ulioagizwa!
Joyce Ndalichako naye ameenda kwenye mfumo uleule tena yeye akisema "utendaji usioridhisha" anathibitisha vipi? Ametumia vipimo gani kuwatia vigogo wa HESLB hatiani? (Nitafafanua jinsi alivyokiuka sheria kuwasimamisha kazi) Ukimsimamisha mtu kazi ni lazima uwe na ushahidi wa dhahiri kabisa! Siyo kukimbilia tu kuchukua hatua!
Rais Magufuli mathalan mkurugenzi wa MNH alimrudisha wizarani baada ya kukosa ushahidi wa moja kwa moja kumsimamisha kazi! Alishajifunza na ndo maana akitaka kumuondoa mtu kwa sasa kunakuwa na mjadala mzito kwanza na wasaidizi wake! Kosa hasa la mkurugenzi wa HESLB ni lipi? Ummy Mwalim alisimamisha watumishi akiwa kwenye kupanga vitanda MNH bila hata kuipitia taarifa ya manunuzi kinagaubaga! Au ndo kutoa pasi ya 'jipu'?
Naona sasa imekuwa fashion lakini serikali itagharamika kutokana na haya!