GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Kwa aina ya Heshima uliyokuwa nayo hasa iliyotengenezwa vizuri kabisa na Marehemu Baba yako ambaye pia alikuwa ndiyo Baba yetu mpendwa wa Taifa Mwalimu Julius Burito Kambarage Nyerere bila kusahau na exposure ya kutukuka uliyokuwa nayo ya mambo mbalimbali jana nilisikitika mno kama siyo sana na aina ya Presentation yako uliyoifanya pale bungeni ulipokuwa unajinadi uweze kuteuliwa tena kuiwakilisha Tanzania kimataifa katika Bunge la Afrika ya Mashariki na Kati ( EALA ).
Makongoro Nyerere Wewe hukuwa Mtu wa .........
Personally nimesikitika mno kwani nina uhakika wa 100% kuwa Wabunge wote wa jana pale walikuamini na hadi kuwa tayari kukupa Kura zao ila walipoona ile poor presentation yako ambayo baadae ilikuja kufunikwa vizuri sana na Mtoto wa Mzee Maghembe ambaye ama hakika Kichwa chake kilijaa ' madini ' tupu na Wao wakaona hawana tena haja ya kupoteza muda na Wewe kwani pengine ungeenda tu kuzidisha ule upuuzi waliouona jana pale huko EALA.
Nakushauri tu Makongoro Nyerere achana na Siasa sasa bali shirikiana na Nduguyo Mzee Joseph Butiku kuweza kuyatangaza ya Baba yako kupitia Mwalimu Nyerere Foundation kwani nadhani Watanzania tunataka kuyajua mengi ya Baba yako ambayo pengine sisi bado hatuyajui au Vizazi vyetu hatuvijui. Kuisaidia Tanzania siyo lazima uwe Mwanasiasa na naamini kupitia MNF unaweza kutufanyia makubwa Watanzania pengine hata ungekuwepo huko EALA.
Nawasilisha na kila la kheri.

- Kuingia ukumbini ' kimzaha ' vile.
- Kuingia ukumbini ukiwa na over confidence ya ' kipuuzi ' vile.
- Kuingia ukumbini na kujielezea ki ' hovyo hovyo ' vile.
- Kuingia ukumbini na muda wote badala ya kujinadi ukawa unaomba tu msamaha.
- Kuingia ukumbini na kujibu maswali ' ndivyo sivyo ' vile.
- Kuingia ukumbini ukidhani jina la Baba yako lingekujenga badala ya kujenga la Kwako.
- Kuingia ukumbini bila ' kujipanga ' vile na ni kama pia ulikuwa umeonja ' brandi '.