Makongoro Nyerere ampasulia JK!

Huyu Makongoro sijui Makhirikhiri ni uharo tu anaouongea.
Baba yake alimshika mkono Mkapa na kutuambia kuwa Mkapa ni mtu safi.

Sasa ana usafi gani kwa mali alizojilimbikizia yeye na mkewe?

Mimi namheshimu sana Mwalimu Nyerere, alifanya mengi mazuri, na uzalendo wake kwa taifa letu hauna shaka.Jambo moja tu ambalo namlaumu huyu mzee ni kutuletea Fisadi kutoka Msumbiji linaloitwa Benjamin William Mkapa na kulipandikiza kuwa rais wa nji yetu.
 

Habari hii niliwahi kuisoma humu siku nyingi sana. Nafikiri, wakati wa kikao kilichowachagua kina Nape
 
Sidhani kwamba JK anashindwa kuchukua uamuzi mugumu kwa kuogopa eti Lowasa atatoa "siri zao", mimi naamini kuwa JK anatumia busara na hatimaye taratibu zichukue nafasi yake ila muda anaouchukua kutoa maamuzi ndiwo unaofanya watu waulize maswali mengi. Nasema hivi kwa sababu, kama ni kweli kwamba wana "siri" nyuma ya pazia, basi siri hii lazima iwe kubwa kiasi cha hata JK awe na kigugumizi asifanye kazi yake ipasavyo mbele ya umma wote na maana yake bila kusubiri ni tayari JK angekuwa na hatia kubwa sawa na usaliti kwa umma ila kubwa kiasi gani mpaka tuijue. JK ana akili tele hawezi ku-risk kiasi hivyo. Hizo ni siri gani tusizoweza kujua maana mchawi anawanga usiku lakini hujulikana. Tuweke subira kudumisha amani.
 
Labda nikuulize hivi..!Wakati mwl Nyerere akimnadi Mkapa mwaka 95 the later alikuwa na sifa gani mbaya ambazo Nyerere alizifumbia macho?Tumlaumu kwa lipi hapa!Kwa kutojua kuwa mkapa atachange on the way?Yeye ni Mungu?Angalau basi mwl Nyerere angekuwepo uchaguzi wa awamu ya pili ya mkapa ungemlaumu.Lakini alifariki mwaka mmoja kabla ya uchaguzi.Hii tabia ya kumchafua baba wa taifa kuhalalisha wizi na ufisadi wa hawa mafia wa kimtandao waliowahi kukataliwa nae inanikera sana..!
 
achana na uzamani tunataka ya leo leo, mustakabali wa nchi yetu huko mikononi mwa Lowasa na family yake!!!
 

Actually bro uko right kabisa kwani madudu haya yote yameanzia kwa Mkapa na kuhamia kwa JK ambaye wa2 walibank on him kama angerudisha nyumba za umma na kuwabana corrupt people in TZ lakini na yeye JK amenushishwa rupia na EL, Chenga, RA na Mr. Ticks. then what do u expect. Hii thread ni bomba sana Makongoro ni dume we need such people in the party not like Kingunge ambaye amekuwa bubu kabisa.
 
Mkapa ndio aliiba hadi Nyerere mwenyewe pia alikosa imani nae,wkt Mkapa alipoleta sera ya ubinafsishaji akaiuza NBC kwa bei ya kutupwa ndipo mgogo-nafsia ulianza kwa Nyerer kuhusu chapuo lake.Pamoja na hayo yote kutokea wakati wa utawala wake,but still he is BEST than JK
 
Haya mi niliyajua na kuyasema tangu zamani, Huyo makongoro nae atasema mpaka atachoka. Huu ndio mwanzo wa mwisho wa CCM
 
Ccm ni usanii na sarakasi kwa kwenda mbele,tutalishwa sound ya kujivua gamba mpaka yesu atakapo rudi,dawa ni kuing'oa tu madarakani by any means.cdm tupeni mwongozo na pia changeni karata zenu vizuri tu kwani kwa upepo huu ndani ya ccm na usanii wanaotufanyia sioni ni kwanini msichukue nchi 2015
 
Huyu Makongoro sijui Makhirikhiri ni uharo tu anaouongea.
Baba yake alimshika mkono Mkapa na kutuambia kuwa Mkapa ni mtu safi.

Sasa ana usafi gani kwa mali alizojilimbikizia yeye na mkewe?

Naamini Makongoro kaongea kama yeye na siyo mjumbe wa Nyerere. Si lazima kujibu post kama huna cha kuandika.
 
Makongoro uliwahi kuwa Mbunge wa Arusha mjini..Sasa unafanya nini kwa Magamba? au Maslah na haki za baba kiserikali unaogopa zisipotee??
 


Mkuu hukunisoma vizuri, sijamchamfua Late Mwalimu, nilitangulia kusema namheshimu kwa mazuri mengi aliyofanya na uzalendo wake kwa taifa letu hauna shaka. Nimelaumu kuwa yeye ndiye aliyetuletea Fisadi Mkapa, hili halina kificho na wala simchafui kwa hilo, ni kosa alifanya na kila binadamu anakosea. Hata yeye mwenyewe kwenye hotuba yake ya Mei Mosi kule Mbeya 1995 alikiri kuwa yapo mengi tu ya "kijinga " waliyafanya katika miaka 23 aliyokaa Ikulu, lakini pia yapo mazuri,alichokuwa anashanga hawa majuha aliowaachia nchi ni kuacha yale mazuri na kukumbatia yale ya kijinga, jee kwa kukiri hivyo alikuwa anajichafua kwa tafsiri yako wewe?


 
Naamini Makongoro kaongea kama yeye na siyo mjumbe wa Nyerere. Si lazima kujibu post kama huna cha kuandika.

Rejea posti yangu vizuri, mimi nimemkumbusha kuwa hata Baba yake alishatutia chaka la Simba na kutuaminisha kuwa Mkapa anafaa.
Usikurupuke kureply usichokielewa.
 

Hapana mkuu!bado naendelea kukataa kwamba 'Nyerere alituletea fisadi Mkapa'!By that time mkapa hakuwa fisadi.Nyerere hakuwa Mungu wa kumtambua Mkapa kuwa atakuwa fisadi baadae.Unafahamu kuwa Mkapa aliingia ikulu akiitwa aka 'Mr.Clean'?Sasa hilo la kutuletea fisadi limetoka wapi?Ndomana nimekuuliza hayo mabaya ya Mkapa wakati akinadiwa na mwl Nyerere ni yapi ili tupate uhakika kuwa Nyerere aliyafumbia macho?Otherwise nakubaliana na wewe kuwa Nyerere hakuwa malaika,kuna makosa alifanya kama alivyokiri mwenyewe lakini hili la "kutuletea fisadi Mkapa"bado nalikataa.Huwezi kulinganisha hilo na Kikwete kuwapigia kampeni akina Mramba,Chenge,Lowasa na Rostam kwakuwa hawa tayari walikuwa ni sehemu ya mijadala ya ufisadi popote nchini na nje ya nchi.Sasa Mkapa as CCM presidential candidate by that time alikuwa na image ipi mbaya kuhusu utendaji wake?
 
Huyu Makongoro sijui Makhirikhiri ni uharo tu anaouongea.
Baba yake alimshika mkono Mkapa na kutuambia kuwa Mkapa ni mtu safi.

Sasa ana usafi gani kwa mali alizojilimbikizia yeye na mkewe?

Usimhukumu mtu kwa "makosa" ya mzazi wake. Istoshe wakati Nyerere anamnadi Mkapa, Mkapa alikua clean bado. Alichafuka baadae
 
nafikiri sasa tumeanza kupata picha halisi ya chama cha magamba. Inanikumbusha moja ya mistari katika biblia "asiye na dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe huyu mama". Mara wote wakatawanyika
ii nimeipenda maselef uko smart, hawa jamaa (ccm) wote ni uhalo kama hawajaoza ili lidubwana e low.. Yawezekana kila likiiba linawapelekea wanagawana na vitambi vinachomoza, na magamba (ccm) wote wanalijua ilo ndo hawawezi kuwa na jipya lolote mbele ya watz. Yani tuna hasira nao za kutosha, ngoja ifike 2015 najua watakuja na upupu wao waloupanga kwa kutumia masabuli yao yasooshwa, ile harufu tu lazima tuwazomee na kuwatoa mbio wallahi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…