Kamamda msome Dr.Slaa kiduchu hapa chini.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao."Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi,".