Magazetini
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 593
- 1,713
Huyu Mhongo sio mwanasiasa haya mambo ya ubunge atayaweza wapi..? Ana majibu ya nyodo na hanaga busara kwenye kujibu hoja za kuudhi.. Hebu arudie mambo yake ya kisomi aliyokuwa akiyafanya kabla ya kuingizwa siasani na JK..
Jimbo la Butiama siyo la Mkono, Mkono yuko Msoma vijijini, jimbo ambalo limegawanywa, jimbo jipya ndo anagombea MuhongoMakongoro anaogopa kumuudhi Mukono, lakini jimbo la Butiama angepita kirahisi. Kawe anahangaika bure, hatopata kitu. kwa ccm.
Huyu ndo atawanyosha mafisadi ya chinichini kama Mengi.
Huyu ndo atawanyosha mafisadi ya chinichini kama Mengi.
Hivi mwananchi wa kawaida anaweza akawa fisadi bila ya mfumo ulioko kuruhusu hilo. Jaribu kuukwepa kodi na hauna wa kukukingia kifua uone dawa yake. Wanyooshane kwanza wenyewe kwa wenyewe halafu uone kama kuna mwananchi wa kawaida atakuwa fisadi sio upande mmoja anajidai mkali na upende mwingine anajipendekeza.
Kwahiyo unataka kuniambia wakati wa uchaguzi mbowe anavyokopesha chama mikopo hewa na baadae kudai na riba ya 100%....tatizo ni mtu mwenyewe au mifumo ya chama?
Kama hili ni la kweli nina hakika hawezi kufanya mwenyewe bila msaada wa wanachama wengine. Jambo zuri au baya linalofanywa na kukubaliwa na watu kadhaa katika chama chochote huo ni mfumo.
Muhongo sijui Magufuli hakuna mtu wanaweza mnyosha kama mfumo wao utabaki ulivyo. Wataishi porojo tu action sifuri.
Tumemuweka Magufuli kwa ajili ya special assignment ya kubadili mfumo...tunataka kurudisha heshma ya chama. Over!