TANZIA Makongoro Mahanga afariki dunia asubuhi ya leo Muhimbili

Hakuna uhusiano kati ya ccm na Mwenyezi Mungu, labda wewe utakuwa ni miungoni mwa wale walioamuru Lisu apigwe risasi huku CCM ikifurahia hilo jambo
Na wewe si msemaji wa Mungu wa kumsemea nani ana mahusiano naye. Our God is a merciful God. Maandiko yake yakuongoze kutambua kuwa hata huyo mpiga risasi inawezekana saa hizi ana mahusiano na Mungu kuliko mimi na wewe tunaoishi na vifundo rohoni.
 
Kwahiyo unataka kusema heshima yake haitopaishwa
Akili nyingi huwa inaondoa maarifa, wengi waliojidang'anya na wale wenye msimamo wa kutokubali kugeuka jiwe maskini wanakufa kwa kihoro wakitazama Mambo yanavyopelekwa na Jiwe. hawaoni mlango wa kufurukuta tena. Pole Milton nakushukuru kijitabuu chako cha warehousing management kilichangia kunipa cheti ADMM NSTI.
 
R.i.p msomi.
Laiti akili ingekuwa inachukuliwa kichwani mwamtu kama memor card kwa kweli kuna memory card tusingeziacha mtu akifa
 
Na wewe si msemaji wa Mungu wa kumsemea nani ana mahusiano naye. Our God is a merciful God. Maandiko yake yakuongoze kutambua kuwa hata huyo mpiga risasi inawezekana saa hizi ana mahusiano na Mungu kuliko mimi na wewe tunaoishi na vifundo rohoni.
Wewe umechanganyikiwa yaani muuaji awe na mahusiano na Mungu wakati hajatoka hadharani kuomba radhi? Hivi kweli unajitambua wewe? Tangu lini Mola akawa na uhusiano na muuaji?
 
Wewe umechanganyikiwa yaani muuaji awe na mahusiano na Mungu wakati hajatoka hadharani kuomba radhi? Hivi kweli unajitambua wewe? Tangu lini Mola akawa na uhusiano na muuaji?
Wewe kwa huyo Mola ni nani bandugu hadi umsemee? Kuomba radhi hadharani kwa mujibu wa maandiko gani!. Ndio Mungu anaweza kuwa na mahusiano na muovu yoyote hata muuaji. Kayasome vizuri ya Mfalme Daudi baada ya kumfanyizia Uriah na kumpora mkewe (Bathsheba) na pia ulinzi aliopewa Kaini baada ya kumshughulikia Abeli.
 
je,kwani ni upi uhusiano wa CCM na shetani??

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni matendo na kauli chafu za wamiliki wa ccm. Mfano, Bashiru Ally (katibu CCM) kusema kwamba watahakikisha ccm inashinda uchaguzi hata kwa kutumia vyombo vya dola(polisi,jeshi nk), Polepole (mwenezi wa CCM) kusema kwamba upinzani ni sawa na corona, Mwenyekiti wa CCM akiwambia wakurugenzi kuwa "Nikupe gari na mshahara halafu umtangaze mpinzani? nk. Haya yote ni ushetani na roho mbaya kabisa hapa Tanzania
 
Akili nyingi huwa inaondoa maarifa, wengi waliojidang'anya na wale wenye msimamo wa kutokubali kugeuka jiwe maskini wanakufa kwa kihoro wakitazama Mambo yanavyopelekwa na Jiwe. hawaoni mlango wa kufurukuta tena. Pole Milton nakushukuru kijitabuu chako cha warehousing management kilichangia kunipa cheti ADMM NSTI.
Ndugu yangu... kwani maisha ni siasa peke yake? Subiri nisiku-challenge sana.... kusema kweli wanasiasa wetu wa Afrika hufanya siasa kama ndiyo ''oxygen'' yao na wanapokosa cheo hujikuta kama samaki aliyetolewa baharini! Nimesoma michango ya watu wengi hapa. Misimamo ya wengi ni kuwa watu wanaoitwa wanasiasa wanatakiwa kupewa kuingiza kipato chao kutokana na vyeo vya kisiasa na hawatakiwi kujishighulisha na mambo mengine yoyote. Hivi kweli msomi mwenye Phd tunamsikitia kwa sababu amesahaulika kwenye vyeo vya kisiasa? Tanzania tumefikia hatua ya kukubali kuwa mtu akishaingia kwenye siasa basi ni lazima apewe vyeo mpaka atakapofariki?
 
Wewe kwa huyo Mola ni nani bandugu hadi umsemee? Kuomba radhi hadharani kwa mujibu wa maandiko gani!. Ndio Mungu anaweza kuwa na mahusiano na muovu yoyote hata muuaji. Kayasome vizuri ya Mfalme Daudi baada ya kumfanyizia Uriah na kumpora mkewe (Bathsheba) na pia ulinzi aliopewa Kaini baada ya kumshughulikia Abeli.
Unajua nini maana ya Agano? Nini maana ya agano la kale?
 
Back
Top Bottom