Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,395
- 13,266
Katika mapokezi ya ndege leo RC Paulo Makonda amesema wabunge wa upinzani hawawakilishi kero na matatizo ya majimbo yao. Ametaja majimbo ya Ubungo, Kawe na Kibamba pamoja na wabunge wake na akamwomba rais ampe bil 1.5 yeye ili awajengee hospitali wananchi wa wilaya ya Ubungo.
Kwa kumkumbusha tu makonda ni kuwa serikali kupitia viongozi wake wakiwemo mawaziri hadi rais wamesema hawawezi kuwasikiliza wabunge wa upinzani. Serikali ndiyo inayokusanya kodi hivyo ndiyo yenye wajibu wa kutoa huduma kama za afya na elimu kwa wananchi kazi ya mbunge ni siyo kujenga hospitali. Sasa kama wabunge wa upinzani serikali imekataa kuwasikiliza na pia kutopeleka miradi ya maendeleo kwenye najombo yao yeye ana haki gani kuwalaumu.
Kwenye jimbo alilokuwa akiliongoza Lissu serikali ilikuwa haipeleki maji kwakuwa tu mbunge ni wa upinzani. Baada ya kuingia wa chama tawala hata kabla mbunge hajaanza kazi rasmi rais akatangaza kuwa atapeleka maji kwakuwa mbunge ni wa CCM.
Naibu waziri wa elimu.akisema alikuwa hawezi kwenda Simnjiro wakati mbunge alikuwa wa upinzani. Baadhi ya ma RC wenzako wametangaza wazi kuwa madiwani na wabunge wa CCM wawapigie simu muda wowote watapokea lakini simu za madiwani wa upinzani hawapokei.
Hata kwenye hiyo shughuli ya ndege mliwaalika viongozi wa upinzani zaidi ya kuwaandaa wana CCM kwa wingi? Tatizo mmegeuza kila kitu kuwa chaCCM. Mnatengeneza utengano ambao baadaye hamtaweza tena kuunganisha watanzania wote kama taifa kwasababu ninyi ndio mnaona mna haki katika nchi hii