Makonda, tembo ukimsifia sana mgema utia maji

Oct 7, 2015
86
108
Maana Hivi Karibuni Tumeona Ukionesha Uwajibikaji Kwenye Baadhi Ya Mambo Ya Kihalmashauri Na Hata Kitaifa.Yapo Ambayo Mh Umefanikiwa Lakini Yapo Ambayo Umezua Taharuki Kubwa Na Hisia Za Ndani Kwa Wale Wenye Kutazama Kwa Kina.

Labda Nikukumbushe Tu Kuwa Baada Ya Kupishana Kauli Na Watendaji Wako Ndani Ya Wilaya Akiwamo Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Kinondoni,Mh Meya Jacob.Ukahamia Katika Suala La Kuwasafirisha Walimu Bure Ndani Ya Jiji La Dar Es Salaam .

Hoja Mabayo Imepingwa Vikali Na Wachambuzi Wengi Wa Kisiasa Na Kiuchumi,Lakini Pia Na Walimu Wenyewe.Sasa Kama Haitoshi Mkuu Umeamua Kutuletea Majizi Katika Wilaya Yetu Ya Kinondoni,Kampuni Ya GSM


KUSOMA MAKALA YOTE FOLLOW THE LINK

MH DC MAKONDA ,TEMBO UKIMSIFIA SANA MGEMA UTIA MAJI | siasa leo tz
 
Mleta mada umeeleweka ulichomaanisha, ila haijakaa vizuri labda kama umefanya makusudi. Hii kitu inasomeka hivi "Mgema akisifiwa, tembo hulitia maji". Mgema ni mgemaji wa pombe inayoitwa tembo kutoka kwenye mnazi, hivyo akisifiwa sana kwamba pombe yake (tembo) ni nzuri, yeye hulitia maji hilo tembo labda kwa maana ya kulifanya liwe jingi na mwisho linaharibika na sifa yake inaharibika pia. Hii ni kutufundisha kwamba mtu asisifiwe sana maana mwisho sifa itamharibu. Rekebisha heading mkuu.
 
Duuu!!! TEMBO UKIMSIFIA SANA, MGEMA HUTIA MAJI. haya ni madhara ya shule ya wanafunzi 500 kuwa na mwalimu mmoja tu.
 
Duuu!!! TEMBO UKIMSIFIA SANA, MGEMA HUTIA MAJI. haya ni madhara ya shule ya wanafunzi 500 kuwa na mwalimu mmoja tu.

Hata mimi nilitaka kusema juu ya shule. Hata hivyo huyu jamaa anaonekana hayuko vizuri katika kufikiri, maana hicho alichoweka kwenye heading hakieleweki. Hizi shule za siku hizi ni shida tupu.
 
Back
Top Bottom