zimwimtu
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 1,988
- 1,095
Kwanza kabisa nikupongeze kwa kuwa na roho ngumu ya kuhimili maneno yote yanayosemwa juu yako, japo kidogo umeanza kulegea.
Ndugu makonda umekuwa machapakazi na mfano wa kuigwa kwa wakuu wote wa mikoa hapa Tanzania. Jinsi ulovyosolve matatizo ya wanainch wakati ule wa ziara yako ya DAR MPYA. Umejenga kituo cha akina mama pale mwananyamala, kwa juhudi zako barabara ile ya kurasini imejengwa kwa kiwango cha zege, kwa juhudi zako, walimu walipata kibali cha kusafiri bure jijini daslam, japo walikataa wenyewe kwa kuogopa kudhalilishwa na makondakta wa daladala. Mambo ni mengi sana lakin nimalizie na hili la madawa ya kulevya ambalo mpaka sasa linatrend. Hakuna mtu alishatokea Tanzania akafikia kiwango ulichofikia katika kudhibiti madawa ya kulevya. Umeweka standard ya juu sana, mateja wamejisalimisha sober house, wauza unga wameishi kwa mashaka, mikoa yote, kwa kufuata mfano wako, wamechoma sana mashamba ya bangi na mirungi.
Japo niwe mkweli kidogo, kwamba approach ulioitumia haiwezi kuwatia hatiani watuhumiwa, kwa sababu inawapa mwanya wa kuficha ushahidi. Lakin impact yake mtaani imeonekana, kweli madawa yamekuwa adimu.
Utendaji wako umedhihilika na hivyo kuwemo kwenye matarajio ya wengi kwamba unaweza kushika nafasi kubwa serikalini hapo baadae, na hii ndo maana imekutengenezea maadui ndani ya chama chako, (ukiachilia mbali wauza unga ambao uliwatangazia vita).
Tunao vijana watatu ndani ya chama chako, (nape mwigulu na january) ambao wanatazamiwa kuchukua nafasi za juu hapo baadae. Kuibuka kwako kunaweza zidisha ushindani katika nafasi hizo za juu, hasa ukizinga umekuwa kipenzi cha mkulu, inawatia wasiwasi sana. Hawa ndio maadui wako wapya. ulimuona nape kujidai yeye huwa anasimamia ukweli, baada ya kuona kusimamia jambo lile la clouds anakuangamiza wewe. Mbona kwenye bunge live alisimamia lisioneshwe? mbona muswada kandamizi wa habari alisimamia mpaka ukapita?? ina maana nape anaamini katika bunge la gizani???
Kwenye suala la VYETI vyako vya kidato cha nne, kwa yaliyosemwa mpaka sasa, na wewe kushindwa kudhibitisha kwamba hujatumia vyeti vya mtu mwingine, ni dhahili una kosa hilo. Ambalo huwezi kulikwepa na ukasimama kwenye majukwaa ya kisiasa.
Ushauri wangu kwako ni kwamba rudisha mpira kwa kipa.
Ongea na mh raisi, achia ngazi, rudi shule. Bado unayo nafasi. Unaweza kusoma QT kwa miaka 2 ukafaulu form IV. Baada ya hapo soma certificate na diploma. 2020 ni mbali utakuwa ushamaliza. Alafu tukutane kwenye majukwaa ya kisiasa 2020. Umtu akiuliza cheti unakionesha, utakuwa umewamaliza. ukishakuwa mbunge au waziri unaweza soma degree sasa kwa wakati wako.
Sisi wanainch bado tutakumbuka utendaji wako, naamini utafanikiwa. Ukiendelea kung’ang’ania madaraka, akiondoka raisi anayekungia kifua akaja mwingine, hutabaki hapo ulipo na ndo utakuwa mwisho wa maisha yako kisiasa.
Do the right thing, bado una muda kwa sasa.
WABILLAH TAWFIQ