Makonda: Rais Samia ametoa Tsh. 2 Bilioni kwa ajili ya Watengeneza maudhui Mtandaoni (Content Creators)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Vipi Content Creator umeshaenda kuchukua mzigo?

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema Wizara imepatiwa kiasi cha Tsh. 2 Bilioni itakayowawezesha watengenezaji wa maudhui mbalimbali mitandaoni kuimarisha kazi zao na kuwaongezea kipato kupitia majukwaa ya kidijitali.

Amesema hayo Januari 29, 2026 jijini Dodoma na kubainisha kuwa, fedha hizo zimetolewa na Rais Samia, kwa lengo la kuyawezesha makundi yote ya watengeneza maudhui ikiwemo katika Sekta ya Utalii, Michezo, Habari, Jamii, Muziki, Filamu na sanaa nyinginezo.

Soma: Makonda: Nitaenda kumlilia Rais Samia atupe Tsh. 2 Bilioni kwa ajili ya vijana wa Online TV na Content Creators

Amebainisha kuwa, zoezi la uandikishaji wa walengwa linaanza rasmi Januari 30 hadi Februari 15, 2026, ambapo watengenezaji wa maudhui wanatakiwa kufika katika ofisi za Halmashauri za Wilaya, Manispaa za Miji na Majiji kupitia vitengo vya habari, ili kuchukua na kujaza fomu za maombi, zikiainisha taarifa binafsi pamoja na shughuli wanazozifanya.

Your browser is not able to display this video.
==

Tanzania Launches TZS 2 Billion Fund to Support Digital Content Creators

The Government of Tanzania has announced a TZS 2 billion (approximately USD 780,000) fund to support digital content creators across the country.

Speaking on January 29, 2026, in Dodoma, the Minister for Information, Culture, Arts and Sports, Hon. Paul Makonda, said the initiative aims to strengthen the creative economy by enabling content creators to improve the quality of their work and generate sustainable income through digital platforms.

The fund, provided by President of the United Republic of Tanzania, Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan, will benefit creators in sectors including tourism, sports, media, social development, music, film, and other creative arts.

Registration for eligible applicants will run from January 30 to February 15, 2026.
 
tanzania Nzima si watapata elfu 30 tu kila mmoja
Umaskini mbaya sana.

Nakumbuka baada ya MO29, nilikuwa sehemu naongea na washkaji fulani, wakawa wanasifia serikali kwa bando za bure walizotoa na nakumbuka walikuwa wanasema sijui na TANESCO nao walitoa units za bure kufidia mitandao kufungwa kwa siku zile za uchaguzi.

Imagine watu wanasahau madhila yote yaliyotokea wanafurahia bando na units za umeme za bure.

Hiyo bilioni 2 kwa mazingira ya Tanzania inaenda kununua ukimya wa watu wengi sana.
 
Katoa mfukoni mwake au ni kodi za wananchi au zimetoka kwenye mauzo ya dhahabu iliyouzwa kutoka BOT?
 
Wamegawa hizo hela ili content creators wasiiponde serikali maana wameteka wee wameshachoka sasa
 
Wanataka kuwanyamazisha wakosoaji mitandaoni.
Wanajua wakikupa pesa yao hutakuwa na jeuri ya kurusha maudhui inayo wakosoa.
Hutarusu comments za kumkosoa mfadhili wako kwenye contents zako.
Wanafuata ule msemo "You should not bite the hand that feeds you".
 
Dhahabu.....
 
Mwanangu hapa ananiuliza mshuwa ehh hivi content creator ndiyo serikali inawapigania vijana na ndiyo wanaona ndiyo jambo kubwa

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…